Jumatano, 11 Aprili 2012

MATUKIO NA PICHA ZAIDI ZA MAZISHI YA THE GREAT KANUMBA

Mahali lilipowekwa jeneza la the Great
Umati wa watu uliofulika Leaders club jana

Kwaya ya Neema ambayo Kanumba aliwahi kuimba
Wasani wa filamu ambao kazi yao ilikuwa ni kubeba jeneza la Kanumba
Mwili wa Kanumba akiwa chumba cha maiti Muhimbili
Jeneza la Kanumba likiwa limefunuliwa
Marehemu Kanumba the great (moto wa volcano) majina aliyopenda kutumia akiwa katika Jeneza
Mgeni rasmi makamu wa Raisi na viongozi wengine pamoja na ndugu wakitoa salamu zao za mwisho
Mwili wa kanumba ukiwa umebebwa
Mpiga keyboard wa Neema kwaya wakati wa msiba
Wapenzi wa kanumba waliotoka Morogoro
Polisi walikuwa na kazi kubwa sana jana kikosi cha mbwa, farasi na polisi wa kawaida wakiimalisha ulinzi
Mkuu wa mkoa na waziri Membe na viongozi wengine wakati wa ibada ya kumuaga Kanumba
Mke wa rais mama Salma kikwete alikuwa ni mmoja wa watu waliohudhulia
Viongozi wakiwa wameshimama wakati wa ibada, mkuu wa mkoa, makamu wa rais, waziri Nchimbi, Mke wa rais
Wasani wa kike wakiingia uwanjani
Wasani wa kiume, Dr Cheni, Steve, Jb
Mama na dada wa Kanumba wakielekezwa na wanakamati
Jeneza la Kanumba The Great likishushwa kaburini
Watu wakiwa wamepanda juu ya mti ili kuona tukio la mazishi
Umati wa watu waliokuwa makaburini


pamoja na picha hapo juu lakini kuna matukio mengi ambayo yalitokea wakati wa mazishi ikiwamo watu wengi kuzimia kutokana na msongamano wa watu akiwamo Wema sepetu ambaye alikimbizwa hospital ya Mwanayamala kupata matibabu, na inakadiriwa watu kama 600 hivi walizimia, vile vile watu wengi walipanda juu ya miti na wengine kusababisha matawi ya miti kuvunjika na kusababisha majeruhi. katika hali isiyo ya kawaida mama mmoja ambaye alienda katika mazisha hayo akiwa mja mzito alijifungua mtoto wa kiume na mtoto kupewa jina la kanumba na kufanya idadi ya watoto 2 ambao wamezaliwa wakati wa maombolezo ya Kanumba wote kupewa jina hilo la Kanumba. pia katika hali isiyo ya kawaida watu walikuwa wengi kiasi kwamba hata vyombo vya usalama kuonekana kuzidiwa lakini hata hivyo walijitahidi na kulazimika kutumia hata nguvu wakati mwingine ili kutuliza fujo zilizokuwa zikitoka hapa na pale. watu wengi walikata kitendo cha kuuondoa mwili wa marehemu bila kuagwa na washabiki wake na hivyo kulikwa na makundi yaliyokuwa yakikimbia na kuimba inasemekana kuna kundi la watu kama 100 hivi walikimbia mpaka katika kituo cha Polisi osterbay na kutaka Lulu atolewe hata hivyo ilibidi polisi kuchukua silaha na tahadhali za kujihami. zaidi ya yote kaburi la Kanumba imebidi lilindwe usiku kucha na polisi ili kuhakikisha usalama wa kaburi. Shughuli zima ya mazishi ya Kanumba imekadiriwa ni zaidi ya sh milioni 100.

KAMA UNA MAONI YOYOTE NIANDIKIE HAPO CHINI AU TUMA UJUMBE KWENYE NO +255 715 033 671, +255 767 033 671 AU FACEBOOK martmalecela

Maoni 1 :

Bila jina alisema ...

kwakweli imesikitisha wengi kutokana alikuwa anapendwa na wote yani siyo wazee wala vijana ila na lulu nae angefikiriwa sababu sidhani kama alidhamiria kufanya hivyo.