Alhamisi, 8 Machi 2012

Wanawake Magomeni wafanya uinjilisti wa kimataifa.


Shalom wote ni matumaini yangu ni wazima leo ni siku ya wanawake Duniani na ninawapongeza wanawake wanaojitambua wao ni akina nani katika jamii na huku wakifuata mwongozo wetu wa kibiblia kuwa Kristo ni kicha cha kanisa halafu mwananamme na anafuata mwanamke. Lakini leo nichukue muda kuzungumzia week la W.W.K lililoisha j2 kwa yale yote waliyofanya wanawake katika kuwaleta watu kwa Yesu. Walifanya uinjilisti wa kimataifa na kutumia mbinu ambayo wengi hawaijui ila ina mavuno mengi. Na nilisha wahi kusikia mbinu hii ilitumika sana unguja zamani ya kuandaa chakula na kuarika watu wakifika wana kula na wanapata na gombo la chuo pamoja na maombezi, wengine ni jumuiya wa wafanya biashara waliookoka ambao nao huandaa chakula katika mahoteli makubwa na kuwaarika wenzao ambao haawajaokoka na kuwa hubilia. Sasa safari hii ilifanyika Maggomeni niwapongeze wale wote walioohusika ikiwa ni pamoja na uongozi wa W.W.K chini ya ushauri wa Mama Mch D kanemba walifungua ukrasa mpya kwa kile walichokifanya na nikapata wazo kuwa kumbe bado ziko mbinu za kuwakusanya watu na kuwahubiria neon la Mungu badala kutumia mikutano ambayo kwa sasa Dar watu wengi hawaendi kwenye hiyo mikutano, na nikaona kumbe hata kamati ya uinjilisti wanaweza kutumia mbinu hiyo na kwa sababu mtu ameokokea kanisani na ameletwa na mshirika inakuwa ni rahisi kuwafuatalia.

Sasa nieleze sherehe ilivyowa kila kitu kilienda chini ya uongozi wa Roho MT kiasi kwamba sidhani kama kuna mtu alijutia muda wake kuwepo pale maana ile ilikuwa zaidi ya sherehe ya harusi maana watu walijaa na kulikuwa na meza na mapambo yaliyopendeza watu nao walikuwa wamependeza na kufanya ndani ya ukumbi wa All Nations Christian Centre kuwa kwa kwa kuvutia mno kulikuwa na wadada kamati ya mapokezi ambao walifanya kazi nzuri kwa kuwapokea wageni toka getini hata mimi nilipokelewa getini maana name nilikuwa mgeni siku hiyo nilikuwa na mwaliko maalumu!, na kamati ya vinyaji na chakula nao wakikuwa vizuri maana watu walipata vinywaji vya kutosha nilimdadisi mbeba soda wakati wa mkupuo wakwanza kulikuwa na soda kama 600 hii ilinishawishi kuona kuwa kulikuwa na watu zaidi ya 600 katika ukumbi huo maana soda nyingine zilikuwa bado zinaletwa. Muongza shughuli siku hiyo alikuwa mama shughuli Mrs Lumelezi kama kawaida yake alichangamsha na tukio lilianza kwa uimbaji wa sifa ambapo praise team ya W.W.K ilifanya vizuri kulishambulia jukwaa baada ya muda ulianza uimbaji wa vikundi na waimbaji binafsi walioalikwa walianza  kwaya kongwe ya Revival ambao walisababisha ukumbi wote kuchangamka wakti wimbo wa kiinjilisti wa Njoni kwangu ukimba na kufanya watu kuacha viti vyao na kutoka mbele kucheza, baadae uliongezwa wimbo mwingine wa Imani ambao nao uliwachangamsha watu kwaya hivyo ambao usiku huo walivyalia sare za kunguru (nyeupe na nyeusi) walisababisha kila mtu kujisikia vizuri nadani ya ukumbi huo, walifuata Anointing soldiers kwa nyimbo 2 na Mwimbaji binafsi Julieti nae aliimba wimbo 1 na baadaye mshauri wa W.W.K Mrs Kanemba aliletaneno kwa upako ambalo mtu yeyote ambaye hajaokoka lilimfanya kujiuliza na kukata shauri, baada ya hapo kilifuata chakula kilichoandaliwa vizuri na dada Jeni kilanga na watu wote walipata chakula. Na mwisho kabisa kulifuatiwa na zawadi zilizotolewa na Mr Kulola ambapo alitoa zawadi ya Yesu maishani mwa watu na kwa kweli watu wote ambao siku hiyo walioalikwa ambao wengi wao walikuwa hawajaokoka walitoka mbele kwenda kupokea zawadi hiyo ya Yesu maishani mwao na yaliendelea na maombezi ambako watu wengi walifunguliwa wwaliokuwa na mapepo.

Changamoto iliyopo ni je? wale wote waliookoka siku hiyo watafuatiliwa kikamilifu maana kuzaa mtoto si kazi kazi ni kulea jinsi walivyoweka nguvu kubwa katika kuanda kusanyiko hilo basi wafanye nguvu katika kuhakikisha kundi kubwa la watu waliokoka wanaendelea kubaki kanisani.

Mc wa Dinner Party Mrs Lumelezi



Revival Choir wakiimba

Bloger akiwakilisha ujumbe kwa njia ya uimbaji

Mama Mch alishindwa kujizuia na kujikuta akiungana kucheza na kwaya

Watu walishindwa kuvumilia nao wakainuka na kucheza wakati kwaya ya Revival ikiimba
Mama Mchungaji Kanemba akikisisitiza jambo wakati akihubiri

ukumbi wote wa kanisa ulichangamka na watu karibu wote kuchea wakati wqa uimbaji huu ni wimbo wa Imani
Kwaya ikiimba wimbo wa pili Imani
Mama Mchungaji akihubili
Charles uzalendo ulimshinda na akatafuta maiki na kuungana kuimba  na kwaya katika wimbo wa Imani

Watu wakipata vinyaji na neno la Mungu wanakula vya mwilini na rohoni

watu wakiwa nadhifu ni zaidi ya harusi wakiendea kupata burudani ya uimbaji

watu wakiwa wametulia wakifuatilia kwa makini kila kinachoendelea

wakati wa kupata vya mwilini ulifika watu wote walipata chakula

John akiwajibika
Anointin wakiimba
Mpiga keyboard Joshua

Vijana wengi wageni siku hiyo walikuwepo kupata burudani na neno la Mungu
watu wakichangamkia chakula
Wa
wahudumu waliojipanda kuhudumia chakula na viywaji



baada ya mambo yote baada ya watu kupokea zawadi ya Yesu walifanyiwa maombezi na watu wengi walifunguliwa kutoka katika vifungo vya shetani

Ayubu Akiwajibika
Watu wakiombewa waliopagawa na pepo
Watu wanafanyiwa maombea na watumishi wa Bwana
Watu wakiombewa
baada ya mambo yote Mr Kulola alitoa zawadi ya Yesu kristo katika maisha ya watu.










Picha za matukio utazipata kwenye facebook ya Kanisa All Nations Christians C.C au fuatilia Martin Photo Galley kwenye blog yangu martmalecela.blogspot.com
picha zote kwa hizani ya MR Daffi

Mathayo 6:33 Utafuteni kwanza ufalme wake na haki yake na hayo mengine mtazidishiwa.

Hakuna maoni: