Jumanne, 6 Machi 2012

JE SHETANI AMEFANIKIWA KIASI GANI KATIKA MPANGO WAKE KWAKO?

Lucifer mkuu wa mashetani aliitisha semina elekezi
kwa mashetani wote duniani na katika hotuba yake ya ufunguzi wa mkutanohuo alisema:-

"Tumeshindwa kuwazuia wakristo wasiende kanisani"" Tumeshindwa kuwazuia wasisome biblia zao na kufahamu ukweli"" Tumeshindwa hata kuwazuia wasiwe na mapenzi ya kweli kwa Mwokozi wao" "Mara wapatapo muungano wa kweli na kristo, mamlaka yetu yatakuwa

yamefika mwisho."" Kwahiyo waacheni waende kanisani, waacheni waendelee na karamu zao za upendo, LAKINI waibieni muda, ili wasipate nafasi ya kudumisha mahusiano na mapenzi ya kweli kwa Yesu Kristo...."

"Hiki ndicho ninachotaka mfanye." alisema
Lucifer:"wataabisheni wasipate kamwe kushikamana na mwokozi wao na wasifungamane naye kwa siku nzima!"
"tutafanyaje jambo hilo ?" mashetani yalimwuuliza kwa jazba.

"hakikisheni wanakuwa 'BUSY' (BUSY= Being Under Satan's York ) katika mambo yasiyokuwa na umuhimu katika maisha yao na muanzishe mipango mingi sana isiyohesabika ili kujaza akili na ufahamu wao,"alijibu shetani "wapeni kutumia, na kutumia, na kutumia; na kukopa, nakukopa, na kukopa." 'washawishini wake zao waende kufanya

kazi kwa siku kushinda huko kwa masaa mengi sana kwa siku na waume zao wafanye kazi kwa siku sita hadi saba kwa wiki, na masaa 10 hadi 12 kwa siku, ili wasiweze kupata nafasi ya kutulia na kutafakari chochote kulingana na mfumo huo wa maisha." "Wazuieni wasiwe na nafasi yakukaa na watoto wao" "Familia zao zikiparaganyika, mara, nyumba zao

hazitakwepa msongamano wa kazi na mawazo." "Wachocheeni zaidi akili na fahamu zao ili kuhakikisha kwamba hawaiskii ile sauti ndogo,tulivu ya Mungu wao."

"Washawishini walize radio au kaseti au muziki kwenye simu,popote wanapoendesha gari au wanapotembea kwa miguu . " waache TV,VCR, CD na KOMPYUTER zikiwa zimewashwa kama kawaida majumbani mwao na mhakikishe kwamba kila duka na mgahawa kote duniani

linapiga muziki usiokuwa wa kibiblia mfululizo bila kukoma." "Hii itasonga akili nafahamu zao na kuvunja ule muungano wa Kristo." "Jazeni magazeti na vijarida mbalimbali kwenye meza zao za kahawa na chai dunia kote." "Shindilieni habari na matukio mbalimbali ndani

yafahamu zao kwa muda wa masaa 24." "Ingilieni kwenye muda wao wa kuendesha barabarani kwa kuwaonyesha mabango na matangazo.' "Kwenye masanduku ya posta na barua pepe jazeni vipeperushi na majarida na kila aina ya matangazo ya habari za vitu na hudumu yanayowapa matumaini ya uongo."

"Wekeni wanawake warembo sana mitaani,club, maofisini na kwenyeTelevisheni na majarida ili kwamba wanaume walioko kwenye ndoa wadanganyike na kuamini

kwamba urembo wanje ndio muhimu, na wasiridhike na wake zao." "wafanye wake zao wachoke sana wasiweze kuonesha upendo kwa waume zao usiku." 'Wapeni maumivu ya kichwa pia!" " kama hawatawapa waume zao upendo wanaouhitaji sana ,wataanza utazama kwingine." "Hiyo itaparaganyisha familia zao haraka sana !" "wapeni waalimu wa uongo ili wawapotoshe wasifundishe injili ya kweli kwa watoto wao na waumini wao."

"Wapeni zawadi na kadi za pasaka ili wasizungumzie nguvu za ufufuka kwa Kristo juu ya hambi na mauti." "Hata katika karamu zao wachosheni sana kwa anasa nakuwafanya warudi wakiwa wamechoka sana " "Hakikisheni wanakuwa 'BUSY' na kusongwa na mambo kiasi kwamba hawapati muda wa kutafakari wema wa Mungu. Badala yake wapeni kutalii

kwenye maeneo ya ajabu,matukio ya michezo, matamasha, kumbi za sinema na video."Wafanye wawe 'BUSY,' 'BUSY,' 'BUSY,! Yaani wasongwe na kusongwa na kusongwa na kazi kwelikweli!" "Na wanapokutanika kwenye ibada zao za kiroho wafanye waingie katika umbea na fitina na kuzungumzia mambo madogo madogo ya umbea na fitina ili waondoke wakiwa na dhamira mbaya zilizochafuliwa." "Jazeni visababishi vingi vya mambo

katika maisha yao ili wasiwe na nafasi ya kutafuta msaada na nguvu za Yesu." "Muda si mrefu watakuwa wakitegemea akili zao wenyewe,wakihatarisha afya zao na za familia zao kwa ajili ya maangamizi yao wenyewe."

"Itafanya kazi" "Itafanya kazi!"Huu ni mkakati kweli kweli !Mashetani yaliondoka kwenye mkutano yakiwa na hamu kubwa sana ya kutekeleza majuku hayo waliyopewa na kuanza kuwafanya wakristo wawe na kukimbia na mambo huku na huko.wakawa na muda mdogo sana kwa ajili ya Mungu wao na familia zao. Wakakosa muda wa kuwaeleza wengine kuhusu nguvu za Yesu kristo kubadili maisha ya wanadamu.

NADHANI SWALI NI JE SHETANI AMEFANIKIWA KATIKA MIPANGO YAKE ?HIYO WEWE NDIYE HAKIMU!!!!!!!!!!je 'UBIZE' au kutingwa na kazi kunamaanisha : kuwa chini ya mkataba au utumwa wa shetani?Mathayo 6:33 Utafuteni kwanza ufalme wake na haki yake na hayo mengine mtazidishiwa.
Chapisha Maoni