Alhamisi, 15 Machi 2012

NI NANI ATAKAYE WASHUHUDIA MACHANGUDOA?

Sifa za Bwana zivume. natumai muwazima kumekuwa na changamoto katika kuhubili injili ya kristo na kuhakikisha kuwa kila kiumbe anasikia hii habari njema ya Yesu kristo. katika utafiti wangu mdogo nilioufanya niligundua kuwa kuna makundi ambayo hayafikiwi kutokana na mazingira waliopo inakuwa ni vigumu kuwahubiria, mara nyingi nimeona wainjilisti wakishuhudia na kuhubiri katika vituo vya mabasi, masokoni, mahospitalini, nk vilevile mikutano ya injili ambaye hapo mwanzo ilikuwa inaonekana inakusanya watu wengi imepoteza uwezo huo kwa sasa hasa katika jiji la Dar es salaam na inatakiwa itafutwe njia mbadala. lakini kuna makundi ambayo kwa njia moja au nyingine ni vigumu kwao kuweza kufika kwenye mikutano hiyo ya injili, mfano watoto wa mitaani, wavuta unga na machangudoa, machangudoa huwa wanabadilisha ratiba zao mchana wana lala na usiku wao wanakuwa macho kiasi kwamba wao kufika kwenye mikutano ni ndoto kwenda na ukisikia changudoa kaokoka basi ujue ni nguvu ya Mungu tu, hivyo kunatakiwa kuchukuliwe hatua za makusudi kukutana na kundi hili. ziko changamoto nyingi katika kundi hili miaka ya nyuma tuliwahi kufanya utafiti na kugundua vitu vingi katika kuwashuhudia machangudoa.
Machangudoa wakijificha wasipigwe picha

  1. unatakiwa uwafuate kwenye viwanja vyao na wanaotakiwa kuongea nao kwa nyakati hizo za usiku ni mwanaume akiwa mwanamke wanaona unawajoki na wala hawatakusikiliza, na mwanaume wanaweza kukusikiliza na kukujibu  maswali yako maana wanajua mwisho wa yote watapata chochote.
  2. kabla changudoa hajaokoka unatakiwa ujue ataishije baada ya kuokoka maana walio wengi wana kazi hiyohiyo tu. hivyo kazi sio ajila kuwe na fungu litakalomfanya mtu huyo maisha yaendelee au sivyo atarudi mtaani kuuza mwili wake ili apate chochote.
  3. mazingila wanayoishi wengi wanaishi kwenye mageto ambapo hiyo kana asipotafutiwa mahali pa kukaa basi kuna uwezekano wenzake waka mvuta na kurudi kule alikokuwa.
lakini vilevile yako mambo mengine zaidi ijambo wengi ukiwauliza watakuambia kuwa wanafanya hivyo kwa sababu ya maisha magumu lakini mtu uliyookoka utajua tu ni utumwa ambao shetani anawatumikisha wengi wanakuwa na nguvu za kipepo na ndiyo maana ukiachilia tu kuwa wanapata pesa ila wao wenyewe bila kufanya tendo hilo wanakuwa hawako sawa sasa utagundua kuwa huo ni utumwa wanatumikiswa.
Machangu wakiwa kazini mitaa ya Sinza

Machangu wako kazini usiku kwao ni mchana na mchana kwao ni usiku ili kuwahubili labda uwafuate usiku kwenye viwanya vyao.

pamoja na sura hiyo hapo juu ila yote kwa Yesu yanawezekana ila swali je nini nani atakaye waendea na kuanda mazingila mazuri ya kumfanya mtu huyo kweli aache kazi hiyo, changamoto hapa ni lazima umtafutie kazi mbadala, na mazingine mbadala na uangalizi wa karibu ambao utamfanya ajisikie vizuri katika maisha yake mapya na kupata mafundisho na maombi na kumfanya aachane kabisa na marafiki zake wa zamani alio wazoea. wakati huo nilipokuwa kwenye utafiti huo nilipata nafasi ya kuonana na mama mmoja ambaye yeye kwa sasa ni mama askofu ya kanisa la TAG ambaye yeye alifanikiwa kuwashuhudia machangudoa na kuwafanya waokoke na kuachana na kazi ya uchangudoa, maelezo yake yalikuwa hivi. baada ya kugundua kuwa alikuwa anaishi na machangudoa mtaa mmoja alianza kufanya maombi ya kuwaombea na kufanya urafiki nao na kuzoeana nao baada ya hapo ilibidi awe anaongea nao mmoja mmoja anasema kuna siku alimchua changudoa na kumwingiza chumbani kwa mume wake. na kuanza kumwambia habari za Yesu tena kwa kuanza kumwonyesha heshima kubwa aliyopewa ya kuingizwa chumba kwa mume wake na wao machangudoa walikuwa wamemzoea huyo mama na walikuwa wakimwita mama. na baada ya mazungumu yule changudoa alikubali kuokoka na kuachana na kazi ya uchangudoa. na mungu hana hiana akaanza kumpa marupurupu ya wokovu dada huyo akafanikiwa sana na kupata nafasi ya kwenda marekani na hadi sasa yuko huko na yuko kwenye huduma ya Benny Hinn.

hivyo iko changamoto ya kuwafikia watu hawa ambao wainjilisti wengi wametuwa hawatoki na kuwafikia kundi hili wengi wamefungwa na nguvu za giza na wamekata tamaa na maisha na kuona bora wafanye biashara hiyo haramu ambayo ina madhala makubwa sana kiroho kimwini na hata kisaikolojia. kama wewe si mwinjilisti basi chukua nafasi hata ya kuwaombea ili Mungu akutane nao na Mungu ainue watu watakaokuwa na mzigo kuwafikia watu hao. Barikiwa.

Mathayo 6:33 Utafuteni kwanza ufalme wake na haki yake na hayo mengine mtazidishiwa.
Chapisha Maoni