Alhamisi, 15 Machi 2012

DAWA WA WAKE WENYE WANAUME WASIO OKOKA HII HAPA


Katika maisha kunakuwa na changamoto kubwa haswa inapotokea labda mke ameokoka halafu mume wako hajaokoka au mme ameokoka mke hajaokoka. Lakini pamoja na hivyo walivyo tunatakiwa tuishi nao na kuendelea kuwaombea ili Mungu awabadilishe maisha yao na hata wakati mwingine wenzi wao huwa wanapata kumshirikisha maneo ya Mungu yamkini ataokoka. Na wakati mwingine inachukua muda unaomba weee bila majibu usikate tamaa. Mama askofu Masawe akiwa anawaombea wanawake ambao waume wao hawajaokoa alisema dawa ni ndogo pamoja na kuwaombea pamoja na kuwahubiria habari za wokovu bado kuna jambo lingine la ziada ili kumsababisha kuokoka nayo ni kumwonyesha tabia njema!. Haijarishi yukoje hata kama ni mlevi mheshimu na umpende na mfanyie mambo yote kwa upendo, mtengee maji ya kuoga. Mpikie chakula kizuri, na mambo mengine ambayo yatampendeza. Alibainisha kuwa wanawake wengine huwa chanzo cha waume wao kutokuokoka kutokana na tabia zao. Tunatakiwa kuwahubiri kwa matendo na matendo yana nguvu ya kubadilisha maisha ya mtu haijalishi wakoje Mungu atawaokoa. Na mtumishi mmoja wa Mungu aliwahi kusema kuwa wanawake ambao wanaoishi na waume wasiookoka Mungu amewaamini sana ili waweze kuwa badirisha maisha yako. Hivyo wewe mwenye mume ambaye hajaokoka ujue Mungu amekuamini na anataka uwe wakili mzuri ili uwakilishe ufalme wa Mungu katika nyumba yako ambayo itasababisha mume wako kuokoka .Mathayo 6:33 Utafuteni kwanza ufalme wake na haki yake na hayo mengine mtazidishiwa.
Chapisha Maoni