Ijumaa, 16 Machi 2012

CASFETA MKOA WA DSM WAJIPANGA KUREKODI DVD LIVE
katika siku za hivi karibuni vikundi vingi vya kusifu na kuabudu vimepata muamko wa kurekodi nyimbo live kama wanavyofanya wanamziki wa nje ya nchi kama Marekani south Africa na sehemu nyingine hakuna asiyeweza kupinga kuwa kwa sasa mziki wa injili unazidi kupanda chart na kufunika hata miziki ya kiduni hapa Tanzania. kuna vikundi ambavyo vimesha fanikiwa kurekodi live akiwapo John Lisu. mala hii praise team ya Casfeta mkoa DSM wamejipanga kufanya hivyo tar 15/04/2012 katika kanisa la CCC. nikiongea na mwenyekiti wa casfeta mkoa alisema maadalizi yanaendelea vizuri na wanaendelea kutafuta wadhamini zaidi katika kufanikisha azma yao hiyo, ni mambo mengi yana takiwa kuandaliwa ikiwa ni pamoja na mavazi gharama za vyombo vya mziki, audio na video shooter matangazo ambazo gharama zake zinaweza kuzidi zaidi ya 50m. hivyo wenye kuweza kuttusaidia kwa lolote tunawakaribisha ili kazi ya Mungu isonge Mbele. lakini jambo jingine alilosisitiza mwenyekiti kuwa watu wajitokeze kwa wingi katika siku hiyo ili waje waone mambo makubwa waliyoanda ni kweli kuwa watu hawana uwezo wa kusafiri kwenda kuwaona Joyours lakini vitu hivyo unaweza kuvipata hapahapa nchini mtu yeyote asitamani kukosa.Wana CASFETA mkoa DSM wakiwa katika sherehe ya kuwaaga wenzao katika kanisa la CCC kwa sasa wanajinoa kwaajili ya kurekodi live.

Mr Milton Mwenyekiti wa CASFETA mkoa wa DSMMathayo 6:33 Utafuteni kwanza ufalme wake na haki yake na hayo mengine mtazidishiwa.
Chapisha Maoni