Jumatatu, 12 Machi 2012

MWISLAMU AOKOKA ACHENI MUNGU AITWE MUNGU

Jana wakati wa ibada umetokea ushuhuda wa ajabu sana nao unamhusu mama yake na Pendo wa kanisa la TAG Magomeni. wiki iliyopita W.W.K walialika watu kuja kupata chakula cha jioni (dinner Party) kilichotoke Pendo alialika watu wa nyumbani kwao ambao ni waislamu wakaja kula pilau na neno la Mungu waliporudi nyumbani baada kama ya siku jpili baba mwenye nyumba akaitisha kikao na kufoka sana kwa kitendo alichofanya Pendo cha kuwapeleka watu kanisani wakati wao ni waislam ikatokea hali ya kumfokea sana na yakatolewa maneno makali sana mpaka yule baba yake akasema akirudia siku nyingine atakuja kupiga kuanzia mchungaji na kanisa zima na maneno mengi yalitolewa hapo. lakini mdada wa Yesu akatulia tu. jana jumapili wakati ibada inaendelea yule mke wa jamaa ambaye alisea ikitokea tena atapiga kanisa zima akaja kanisani na kusalimisha maisha yake kwa mwanaume wa wanaume Yesu kanisa zima lilifurahi na matuda ya ushuhudiaji wa kutumia chakula unaanza kuzaa matunda naamini wengi watakuja maana kuna mbegu imepandwa mioyoni mwao. jina la bwana libarikiwe

Mathayo 6:33 Utafuteni kwanza ufalme wake na haki yake na hayo mengine mtazidishiwa.
Chapisha Maoni