Jumatatu, 12 Machi 2012

AINA MPYA YA WIZI WA PESA KWENYE MITANDAO YA SIMU

Siku za hivi karibuni wezi wabuni njia mpya ya kujipatia pesa kupitia mtandao wa simu tafadhali chukua tahadhali kama utapigiwa simu na mtu usiye mfahamu usitoe siri zako. yako matukio matatu ambayo mitakupa ambayo yatakupa kujua ujanja wanaotumia yafuatayo nia maelezo ya mhanga wa technolojia akielezea jinsi alivyoibiwa hela kwenye akaunti yake. Leo yamenifika, na ninapenda kutoa tahadhari hii kama hili halijawahi kukumba. Leo asubuhi kuna jamaa alinipigia simu akidai kuwa anatoka kitengo cha NMB mobile banking akaniambia kuwa airtel wanatoa bonus kwa wateja wazuri wanaotumia service hiyo. Sasa bila kujua hili wala lile nikatoa taarifa za simu yangu na hata za account yangu.
Guess What?
Baada ya muda nikarealise kuwa line yangu imekuwa blocked na ndipo niliposhtuka na kujua kuwa nimeliwa!
Nilipiga simu kwa Bank Manager na kumweleza suala hilo na baadaye alinidhhirishia kuwa account yangu imekombwa yote. Hivyo nikamwambia wai-block, kitu ambacho pia kilikuwa kinawapa shida kwa sababu line ilikuwa imeshachakachuliwa. Kama isitoshe, wakaanza kupiga simu kwa watu ambao awali walitaka niwape namba tano za watu ninaowapigia simu mara kwa mara, wakiwataka hao watu wanitumie pesa na kwa sababu simu ilionyesha kuwa inatoka kwangu wengine walikuwa karibu waanze ku-act.
Kwa hiyo ni kuwa zile information za simu yangu ziliwasaidia ku-disable line yangu toka kwenye simu card yangu na na kuziweka kwenye simu card yao maana pia walihitaji ICC number ya sim card yangu, hivyo kuweza kuwasiliana na watu waki-impose kuwa ni mimi. Pili details za benki ziliwapa access kwenye account yangu na kuikwangua yote.
Kwa hiyo ndugu, kama hujawahi tokewa na hili au ulikuwa unalisikia tu kwa mbali leo hii mimi ninakuwa shahidi kwako na tafadhali usotoe taarifa zako zozote kupitia simu kama nilivyofanya mimi. Teknologia ina faida na hasara zake kwa hiyo siyo mbayo kushiriki vyote ila pale iwezekanapo jaribu kuepuka hasara. Kama utataka kujua mbinu waliyotumia unaweza kuuliza nikujuze ili uwe makini kitokea mtu akakupigia simu kama hiyo.


tukio la pili ni hili kutoka kwa jaama ambaye ilibidi asambaze ujumbe huu ili wengine wasiibiwe
Ukipata msg yeyote toka line yangu ya tigo tafadhali usiifanyie kazi. Line yangu ya tigo ilikuwa swaped na mtu asiyejulikana kuanzia juzi saa kumi mpaka jana saa kumi na mbili na ameifanyia uhalifu wa fedha mpaka niliporipoti tigo na kurudishwa kwangu. Leo tena saa tano kamili imekuwa swaped mpaka sasa hivi na anafanya uhalifu wa fedha kwa kuomba contacts wangu watume tigo pesa kwani nina shida za... haraka, wapo waliotuma. Tigo hawajanipa ushirikiano wa kuridhisha na inashangaza kuruhusu mtu kuswap namba (online) pasipo uthibitisho dhahiri. Na kitendo hicho kujirudia mara mbili licha ya kuripoti na kuwaomba waiblack list namba yangu. Iwapo umepoke ujumbe huo tafadhali usiufanyie kazi bali wasiliana nami ili niwasilishe malalamiko yangu kisheria. Poleni

na tukio la tatu lilimtokea mama mmoja hivi karibuni kaa chonjo
. mama mmoja alifika kariako na kuwaomba watu wenye miamvuli wamwingizie hela kwenye simu yake. yule vendor alichofanya alimwambia yule mama ampe simu yake na baada ya kumpa kwa ujanja wa hali ya juu bila yule mama kujua kinachoendelea jamaa aliandika no yake ya simu na kusevu jina la tigo pesa baadae alimwambia yule mama ampe pesa na jamaa akamtumia yule mama msg kuwa amepokea kiasi 30000 kutoka wakala jina la uongo na alivyotuma ile msg ikaingia kwa yule mama na yeye alipoona ile msg hakuwa na shaka maana amezoea kuona msg kama hiyo hiyo yule mama akaondoka alipofika sasa huko alikotaka kutoa pesa zake kuulizia salio hakuna hela na ilichukua mda kujua kilichofanyika jitahidi kuuzia salio lako unapoweka hela kabla hujatoka kwa wakala.

technolojia ina uzuri na ubaya wake ukiachilia mbali wizi wa kwenye mtandao wa simu kuna wizi unaotokea kwenye ATM nao unafanyika hivi kuna watu wankuwa na kamera ndogo ambazo nao huingia kwenye ATM na kujifanya kuwa ni wateja kumbe siyo wanainatisha kwenye mashine kuelekea no ili aweze kuona njinsi watu wanavyoingiza password zao na baadae anatoka na kukaa mbali kidogo kwa mda furani baadae anakuja na anaingiza kadi yake maalumu na kutumia password ambazo kamera imezisoma na kuweza kuangalia salio na kuchukua pesa zote, na kukuacha mweupe pee, hivyo jitahidi kama unatumia card ya ATM jitahidi kabla ya kuchukua hela angalia mashine ya ATM na kama ukiona kuna kitu ambacho sio cha kawaida toa taarifa ili usaidiwe mara nyingi karibu ATM zote zinakuwa na askari watakusaidia kujua kilichopo ni nini.

jitahidi kuwa mdadisi wa mambo ili kujirizisha katika mazingila uliyopo kuepusha usumbufu.

Mathayo 6:33 Utafuteni kwanza ufalme wake na haki yake na hayo mengine mtazidishiwa.
Chapisha Maoni