Jumatatu, 20 Februari 2012

Ufunguzi wa kanisa la Mch Thadeo (Midizini Healing Center)

Tawi jipya la kanisa la TAG Magomeni limefunguliwa jana Tar 19/02/2012 ambalo litaongozwa na Mch Thadeo, kabla ya ufunguzi huo ulifanyika mkutano wa ndani wa injili ambao uliandaliwa na kanisa la TAG Magomeni ambapo mwinjilisti chipukizi Ev Nelson Kazimoto alihubiri siku zote za mkutano na usiku kulikuwa na cinema ya Yesu ilikuwa inaonyeshwa ambayo nayo ilikusanya watu wengi, katika mkutano huo Mungu alionekana kwa kuponya na kufungua waliofungwa na watu waliokoka, ufunguzi wa kanisa hilo unafanya kanisa la Magomeni kuwa na matawi yasiyopunguwa 6 ambayo ni Mch Steven, Mch C Lijongwa, Mch Kabanda ambaye yeye ana makanisa mawili wote hawa wako Tabora na  Mch J. Linde kigogo, Mch Mshama Tandale, na Mch Thadeo ambaye ameanzisha Midizini. na bado mpango wa kanisa ni kufungua matawi zaidi na kuwapeleka watu katika vyuo ya Biblia na chuo cha kupanda makanisa ili kutimiza mpango mkakati wa TAG Taifa wa miaka 10 ya mavuno. niliongea na Mwenyekiti wa kamati ya uinjilisti ambae alisema mwaka huu wanategemea kufanya mkutano mkubwa Tabora kwa Mch Kabanda mwezi wa 6 na mikutano mingine katika matawi ya kanisa.

zifuatazo ni baadhi ya picha za matukio hayo


Washirika wa midizini wakiwa katika ibada ya kusifu na kuabudu jpili ya kwanza ya ufunguzi wa kanisa.

Mch kiongozi wa Midizini healing center ndg  Thadeo akihubiri katika ibada ya ufunguzi.

Wanakwaya wa Revival kutoka TAG Magomeni wakiongoza kipindi cha kusifu na kuabudu na ilihudumu na kwenye mkutano uliofanyika hapo Midizini

Kipindi cha sifa.
Mathayo 6:33 Utafuteni kwanza ufalme wake na haki yake na hayo mengine mtazidishiwa.
Chapisha Maoni