Ijumaa, 17 Februari 2012

Rose Mhando Apata Mkataba Mnono, awapita hata akina AY, FA, NK


Hivi karibuni kampuni ya kusambaza kazi za waimbaji duniani ya Sony imeingia mkataba na muimbaji wa nyimbo za Injili rose mhando kwa muda wa miaka mitano. kampuni hiyo ambayo makao yake ni Africa kusini ilimtangaza Rose mbele za wadau mbalimbali wa mziki wakiwapo wanahabari wanamziki ya bongo fleva, waandaaji wa mziki na wadau wengine katika hotel ya kitali ya kilimanjaro. kuchaguliwa kwake kulitanguliwa na mchakato wa kutafuta waimbaji ambapo kati ya watu zaidi ya 130 hivi walifanyiwa mchujo na kupatikana mtu mmoja mchakato huo ulihusisha na matoleo ya kazi zake ambazo alisha toa na mauzo aliyofanyika katika kazi zake za zamani ambapo kuna toleo ambalo aliwahi kuuza copi 5,000,000. hiyo mkataba alioingia utamfanya azunguke nchi nyingi zaidi ndani ya Afrika na nje ya Afrika kufanya huduma hiyo ya uimbaji. tarifa za wandishi wengi zimesema kuwa huu ni mkataba wa kwanza waimbaji wa nyimbo za injili kufanywa na kampuni kubwaa ya kimataifa ya Sony hapa nchini, lakini huko nyuma mwimbaji mwingine wa nyimbo za injili Pendo Kilahilo naye alisha wahi kuingia mkataba na kampuni hiyo ya Sony alipokuwa Sauth Africa na kubadilisha baadhi ya nyimbo zake na kuimbwa katika Lugha nyingine zaidi ya kiswahili kuwa za kimataifa zaidi ili kupata soko zaidi. kupata kwa nafasi hii kwa Rose inaleta changamoto katika tasnia ya nyimbo za injili na kufanya watu wajue kuwa kuimba ni kazi kama kazi nyingine ambazo kama mtu atakuwa siliasi basi atatoka kimaisha


Rose Mhando akiwa amekumbatiana na Bahati Bukuku baada ya kutangwa na kuingia mkataba mnono na Kampuni ya Mziki ya Sony.

Rose ambaye anatamba na albamu yake ya utamu wa Yesu amekuwa akifanya vizuri na kusababisha mziki wa injili kuwa na soko hapa nchini tofauti na mziki mingine hata kuwafanya wana mziki wa kidunia kuvutiwa na hata wengine kurekodi nyimbo za injili kama alivyofanya Mr Nice ambapo mwishoni mwa mwaka jana alitoa albam yake ya nyimbo za injili na huku yeye ni mwimbaji wa dunia na hata baadhi ya wanamziki wa kidunia nilioongea nao wanasema siku hizi nyimbo za ijili zinapigwa sana kwenye sherehe kuliko nyimbo zozote ha kwenye sherehe za kislam na waslamu wengi nao ni wadau wazuri wa nyimbo hizo wengi wananunua cd na hata kuweka nyimbo hizo kwenye simu zao. vilevile Rose aliwahi kuwika kwenye albamu zake za zamani na ile kiatu kivue aliyoshirikishwa. aidha albamu yake ya jipange sawasawa inaongoza kwa kuuzwa katika albamu zake kwa zaidi ya copi 5000,000. albam yake 1 tu ndiyo haikufanya vizuri katika soko nayo ni zawadi ya krismas ambayo ilikuwa ya pili kutoa baada ile ya kwanza, vile vile Rose amewahi kuwika katika albam aliyolekodi na kwaya ya cimuli Anglican Dodoma na kuna single kadha ambazo amerekodi katika haleluya collection.
Madam Lita akiongea jambo kwenye mkutano huo na nyuma anaonekana mtayarishaji wa mziki wa bongo fleva ambaye haamili kilichotokea

Rose akiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya wanamziki maaruufu wa bongo fleva kutoka kulia ni mwana FA, AY, Daimond, Rose, Bahati Bukuku, Mwl John Shabani.

ninamuombea Rose ili aweze kuwakilisha vilivyo katika mkataba huo alioupata ambao naamini umefungua ukrasa mpya kuonyesha hata nyimbo za injili bado zinaweza kuwa juu hata kufanya makampuni ya nje ya nchi kuona unafaa kusambazwa duniani ukiachilia mbali hizi kampuni za hapa kwetu ambazo huishia hapa nchini tu na bado hawana uwezo wa kutosha kutangaza kazi za waimbaji kimataifa. Mungu mbariki Rose \Mungu wabariki waimbaji wa injili wa Tanzania.
Mathayo 6:33 Utafuteni kwanza ufalme wake na haki yake na hayo mengine mtazidishiwa.
Chapisha Maoni