Pia kulikuwa na tukio la mabomu ya gongo la mboto ambayo nayo yalipoteza maisha ya watanzani achilia mbali lile la mbagala lililotokea mwaka jana. Kutokana na hili tukio kutokea usiku lishababisha watu kukimbia hovyo na hawakujua wakimbilie wapi. Na hiyo ilisababisha majeruhi na vifo vingi na baadhi watoto kupotezana na wazazi wao au ndugu zao. Tukio hilo lililotokea February 16 usiku lilitokana na ghala la silaha za jeshi la wananchi kulipuka na kusabasha dhahama.
|
Hii sio radi bali mabomu yakionekana kwa mbali yakilipuka huu ni usiku wa tar 16 Febr |
|
watu wakishangaa bomu |
Pia kulikuwa na ajari nyingi zilizopoteza maelfu ya watu na kusababisha ulemavu kwa baadhi ya watu katika ajari kuna kikundi cha Taarabu ambacho kilipoteza wasani wapatao 13 katika ajari mbaya sana pale Morogoro. Na ajari nyingine ya kusikitisha sana ni ile ya kuzama kwa meli kule nungwi Pemba ambapo mamia ya watu wakifa maji huku kukiwa na jamaa mmoja amabaye yeye na ndugu zake wapatao 60 walikuwa wakienda kwenye harusi kutoka unguja kwenda Pemba walikufa huku akiwaona na kushindwa la kufanya. Inasikitisha sana, na kuna baadhi ya familia walikufa wote huku nyumba zao zikibaki zimefungwa tu maana hakuna aliyebaki!.
meli ya MV Space Islander ikiendelea kuzama na ilifika kina cha futi 300 na kushikana kabisa kuifikia huko iliko kutokana na kuzama katika kina kirefu
|
Mhanga akiokolewa katika meli iliyozama ya MV Space Islander
Itaendelea ...... |
Mathayo 6:33 Utafuteni kwanza ufalme wake na haki yake na hayo mengine mtazidishiwa.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni