Shalom
washirika wote wa magomeni TAG tunaombwa kuwasaidia wezetu wapatao 40 waliokubwa na mafuriko yaliotokea mkoani Dar. ombi hili limetolewa na Mch kiongozi D. kanemba na kusisitiza kuwa siku ya c- max kila mtu aje kanisani na kile alicho na uwezo nacho ili kuwasaidia wenzetu waliathirika na mafuriko. Mahitaji hayo ni kama ifuatavyo, chakula mf mchele, unga, sukari,majani ya chai, chumvi,maharagwe,mafuta ya mboga,viazi nk na vitu vingine ni kama nguo, maji, sabuni, vyombo ya ndani, au hela taslimu. kuna watu wapatao ishirini mpaka sasa ni homeless wengine wamehifadhiwa kwa majirani wengine wako kwenye nyumba za kulala wageni, na wengine kama 15 hivi wako kanisani wao na baadhi ya vitu vichache walivyookoa na hawana chakula wala vitu vingine vilivyo tajwa hapo juu shime tuungane kwa pamoja ili tuwasaidie wenzetu maana sisi ni mwili mmoja na tunatakiwa kuchukuliana nao katika kipindi hiki kigumu. tunachomshukuru Mungu kwa kweli amekuwa mwema hakuna hata mshirika mmoja aliyepoteza maisha. hapa chini ni baadhi ya familia zilizokubwa na mafuriko.
1.Michael Mwaituka Mzima wao walitoka kama walivyo vitu vyote vilizama kenye maji na ukuta wa nyumba yao umebomoka
2.Mzee mwakyusa na hii imemsababishia fresha kupanda na sasa amelazwa Mhimbili
3.Mch Mshama
4.Mch Linde
5.Mama Patrick
6.Mrs Hilda Charles
7.Shemasi Joseph Madeje
8.Shemasi Kobelo
9.Familia ya Makaranga
10.Dada Mage mwalimu wa watoto
11.Grace Shirima
12.Mr Chitadu
13.Mrs Selina Jackson Muuza chapati
14.Mume wa Zena
15.Mzee Chemponda
Na wengine wengi ambao majina yao hayajaweza kupatikana mara moja kama unataka kutuma pesa tuma kwa mpesa 0767 033 671 begin_of_the_skype_highlighting 0767 033 671 end_of_the_skype_highlighting
Mungu akubariki kwa kuitikaia wito huu wa mchungaji kiongozi D Kanemba kwaajiri ya kuwasadia wenzetu--
Martin S. Malecela
Gari likiwa limetumbukia katika daraja lillilobomoka |
Jeshi la wananchi wakiwa kazini kuokoa waathirika |
Nyumba zikiwa zimezama eneo la Jangwani |
Mafuriko eneo la Jangwani na habari nilizoziona kupitia gazeti la mwananchi inasadikika watu 30 wamepoteza maisha kuanzia mafuriko yaanze |
.http://www.youtube.com/watch?feature=player_embedded&v=r9oGyGgQ-pY
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni