Tumebakiza siku chache ili kumaliza mwaka wa 2011 na kuukaribisha mwaka mpya wa 2012 huu ni wakati wa kufanya tathimini katika malengo yetu tuliyokuwa nayo mwaka huu na kuona tulifikia malengo na kama tulifikia malengo jina la Bwana libarikiwe sasa panga malengo mengine ya mwaka ujao. la kama hatukufikia basi ni wakati wa kutafakari na kuangalia kikwazo kilikuwa ni nini mpaka kutokufikia mafanikio na kutafuta namna ya kutatua tatizo ili kufikia mafanikio. Na kikubwa ni kufahamu kuwa kuanguka sio mwisho wa safari kinachotakiwa ni kuamka na kusonga mbele. Na kukabiliana na changamoto zilizoko mbele yetu. Katika mwaka huu unaoisha kulikuwa na changamoto nyingi sana za kijamii, kisiasa, kiroho nk. Kwa kifupi tu nitajaribu kukumbusha mambo ambayo yalijiri katika mwaka huu.
Katika mwaka huu kumekuwa na mambo mengi yaliyotokea nianze na cup of life au kikombe cha babu wa Loliondo hili liliteka sana fikira za watanzania wengi wakubwa kwa wadogo na kusababisha soleni ambayo haijawahi kutokea Tanzania wakati wowote ule hata kusababisha serikali kuingilia kati na kupanga utaratibu wa watu kufika kumuona babu hii ilitokana na yeye kudai kuwa ameoteshwa na kuonyeshwa dawa inayoponya mgonjwa mengi tena yale sugu. Hili liliwakumba hata viongozi wetu wengi na wengine walienda kwa siri ili wasijulikane kuwa nao wameenda kupata kikombe. Kufanikiwa kwake kulisababisha na watu wengine nao kujitokeza na kusema kuwa nao wameoteshwa na kuanza kutoa tiba kama hiyo hiyo. Hili liliibua utata mkubwa katika fahamu za watu na kusababisha watu kujiuliza maswali kuwa sasa ni yupi mkweli. Kama kawaida viongozi wa dini nao hakulifumbia macho wako waliowakataza washirika wao kutokugusa au kunywa kikombe hicho cha dawa waliyoifananisha kuwa haina tofauti na dawa zingine za kienyeji lakini na wapo waliowaruhusu washirika wao wanywe nahii ilitokana na kutofautiana kiimani.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni