Ni wiki sasa baada ya uchaguzi mdogo wa Igunga na mgombea wa CCM kuibuka mshindi. Sio vibaya leo nitoe changamoto kwenye upande wa siasa maana maisha hayo nayo yanatuhusu ten asana maana kama siasa zitakuwa za vurugu basi hata uhuru wa kuabudu utatoweka. Mimi nianze na kusikitika kwa jinsi uchaguzi huo ulivyofanyika ijapo ulikuwa ni uchaguzi mdogo kama walivyouita wao lakini mimi nasema haukuwa mdogo kutokana na kundi la kubwa zilizotumika. Mimi nilichoona kuwa kundi la watu wachache ambao wao wanatumia ghalama zozote ili wawekane madalakani ili kujinufaisha wao.
Kwa maisha ya mtanzania wa kawaida si lahisi kupanda ndege hata siku moja kutokana kutokuwa na uwezo wa kufanya hivyo lakini leo vyama vya siasa vinafanya kampeni kwa kutumia mahelkopita wamepata wapi hela hizo! kinachonishanga hela kwaajili ya kampeni ipo ila hela kwajili ya kutatua matatizo ya wananchi hakuna yaani kuna shule hazina madawati vitabu, mahospitali hayana dawa n.k ila kumtafutia ulaji mtu mmoja ili awe mbunge wanatumia hela zote hizo, hivi mtu mmoja na wengi bora nini? lakini hawa viongozi wanajijali wao wenyewe. Sasa ghalama lilizotumika katika kampeni nani analipa ningekuwa na uwezo ningekataa mshahara wangu usikatwe kodi maana kodi hizo haziwafikii walengwa bali zinaishia kwenye mikono ya watu wachache tu, na wananchi kubaki na vumbi tu za chopa zinaporuka.
Ghalama zilizotumika kurusha mahelkopta zikijumlishwa kwa vyama vyote zisingeweza kutumika kutatua baadhi ya matatizo ya wana Igunga? Lakini mmewaachia vumbi tu la mahelkopta na magaari yenu na wananchi wanabaki kama walivyo hivi kama Nyerere angekuwepo angekaa kimya kuona hizo ghalama kubwa kwenye uchaguzi mdogo na hali nchi yetu ni maskini kama sio kuongeza umaskini ni nini, kama inayotumika katika kampeni ndiyo ingekuwa inatumika kutekeleza ahadi viongozi wanazotoa Tanzania ingekuwa mbali kimaendeleo. Lakini mmmh wanajali kula yao tu na si wananchi. lakini ni kweli watu wote walikuwa wakijaa walikuwa wanafuata maneno ya wagombea au walifuata kuana chopa jinsi zilivyo zinatua na kuruka mahali popote maana hata mimi ningeshanga sana hizo chopa na nikitoka hapo sikumbuki alichosema mgombea bali kusema habari za chopa jinsi zilivyo zinatofauti gani kati ya chama hiki na hiki maana ni mambo mageni kwao!.
Hivyo basi wanaigunga kwanza poleni kwa pilikapilika za uchaguzi katika jimbo lenu lakini mnatakiwa kujua sasa mtakiwa kulipa gharama za uchaguzi kwa ipi mi sijui, maana ujue mtu anapodhamini kitu ujue gharama zake lazima zirudi na faida juu si bure.
Chopa zikifanya kazi za kampeni huko Igunga picha ya chini watu wakiwa wameizingira chopa hapa nafikiri kila mtu anatanga angalau aliguse tu ili apate cha kusimulia lakini si kusikiliza mgombea. |
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni