Ijumaa, 7 Oktoba 2011

Pongezi sikukuu ya Vijana kutoka kwa Mch Kanemba

Ubarikiwe mwana habari wa CAs. na mwenyekiti mstahafu hii inapendeza sana kwa utukufu wa Mungu!
Nilikuwa najiandaa na masoma lakini umakini wa picha hizi zilizolenga matukio muhimu na jinsi ulivyoripoti
niliona vyema nichukue muda kidogo kuangalia na kumtukuza Mungu kwa jijnsi mambo yanavyokwenda TAG Magomeni.

Jambo zuri ni budi lipongezwe, na Mungu akuzidishie upendo huo na juhudi yako katika kuripoti matakatifu kama hayo, yenye kumpatia Mungu wetu utukufu. MAANA SISI TULIO UPANDE WA MUNGU TUSIPO MTANGAZA YESU KWA MAZURI YAKE, NI NANI BASI ATAFANYA HILO, SHETANI? LA HASHA, NI ADUI WA MUNGU.
Basi tudumu katika kutenda mema katika shina la upendo na Mungu wa Amani aliyemfufua Bwana wetu Yesu Kristo toka kwa wafu AWABARIKI SANA.


Mch Kanemba.
Chapisha Maoni