Jumatatu, 10 Oktoba 2011

MAONI YA :- WANAINCHI WA IGUNGA SASA NI ZAMU YA KULIPA GHARAMA ZA HELKOPITA

Kweli kaka

Sent from my iPhone
On Oct 9, 2011, at 13:36, "Samuel Sasali" wrote:

Kwanza nikupongeze na ujio wako wa kiuana harakati zaidi na sio mtazamo wa siasa lakini kulaumu vyama vya siasa kutumia helikopta na kuacha kuwahudumia wananchi ni matokeo mbovu wa watanzania tulio nao na vyama vya siasa vinadondokea humo. Kwanza Martin nikuongezee mtazamo tuko kwenye dunia ya kibepari dunia ya kutanguliza wengine imeshaisha sasa ni ubepari.
Nikirudi kwenye mada kwanini tuwalaumu ccm,chadema na cuf kabla ya kujitazama sisi wenyewe?
Kwa kuanza ngoja nikuoneshe haya mambo kwa mapana yake.

Sisi wenyewe tumewahi wasaidia wangapi tunaokutana nao? je wale ombaomba tunapowanyima cha kuwapa ni kwa sababu hatuna hela?no sababu hatuwekezi kwa ombaomba sababu hatuna direct return ya ombaomba je hatuwasaidii wale wale wanaotunufaisha tu? vyama vya siasa ni matokeo ya maisha yetu.

Mfumo wenyewe wa makanisa ni kama vya siasa mara ngapi makanisa yamewahi wasaidia walio wahitaji?mchungaji tuna mpa kila wiki hela ya mafuta na kuna mtu anakosa 300 ya nauli ya kurudia nyumbani kwanini unadhani hatuwasaidii wale?tumekuwa na siku maalum za kuwapongeza wachungaji na kuwa nunulia magari mapya while kuna mtu anakosa ada ya mtoto wake vyama vya siasa ni matokeo ya mfumo wa kanisa, kanisa likipinda nchi inapinda si watu wa Igunga tu wanaolipa gharama ila kila mmoja wetu kwa namna moja ama nyingine analipa gharama.

...//Papaa

"Tusijisifu kwa mbio tulizonazo tuwasifu na wanaotukimbiza"

Hakuna maoni: