Alhamisi, 6 Oktoba 2011

MAONI YA WASOMAJI WIKI YA NENDA KWA USALAMA.

Shalom Kanisa,




Mimi nimekuwa nikiwaza siku nyingi juu ya kadhia hii inayopunguza idadi ya mavuno ya wanadamu ambao ilikuwa waokolewe kwa njia ya injili ili watumike ktk shamba la Bw na pia kuwa kama wapiga kura na wachangiaji wa maendeleo kwa upande wa Kaisari, na ninachofiki kifanyike ni haya hapa ktk namna 2 za kiroho na sheria:-



KIROHO.

Kuanzishwe utaratibu wa huduma ya injili na maombezi ndani ya vyombo vya usafiri husika e.g. gari moshi, mabasi na vyombo vya baharini. SUMATRA, EWURA na mamlaka za TRL, BUS TERMINALS na BANDARI zinakotia nanga vyombo vya baharini wahusishwe ktk hili. Wamiliki wa vyombo wabanwe kuwa wahubiri hawa wapende wasipende lzm wawepo kwa ajili ya huduma hiyo muhimu na wasitozwe nauli km wale wanaouza maji na sweets kwenye mabasi ambao wanaweza toka na basi Chalinze mpaka Korogwe na kugeuza na linalotoka bara bila kulipa nauli lkn wakiuza bidhaa zao ndani ya basi.



Kuwepo wahubiri waliotawazwa/waliowekwa wakfu ambao ikiwezekana ili kuepuka mgongano wa madhehebu, vyombo kama TEC na CCT ndiyo vipewe kibali cha kuwateuwa hao watumishi ambao watapangiwa kuwemo ktk kila chombo mara kinapoondoka kuanza safari ambapo kazi yake kubwa ni kushusha tsunami ya maombezi na injili ya dhoruba kuu. Anaweza akaondoka na basi Dar mpaka lbd Chalinze au Mombo, na pale anabadilishana na mwenzake aliyeanzia A-taun [wana swap mabasi]



Mumo humo wakusanye sadaka kwa mtindo wa coupon ili sadaka zidhibitiwe zinapoletwa kanisani kwa mtindo ule wa makusanyo ya Parking System. Pia wanawezakuwa wainjlisti 2 kila basi/meli/boti/treni. Natamani ningekuwa na uwezo basi huduma hii MH tungeianzisha sisi kwa sababu MH wamesambaa nchi nzm hii. Ila tutaachaje kazi za Kaisari?! Watoto wa mamdogo km wakihitaji basi na wao waanzishiwe ya kwao kupitia BAKWATA,



KISHERIA.

Kuna haja ya kuanzisha road surveillance ya chopper ya polisi km inavyofanyaga wakati wa chaguzi [hata juzi ilirushwa kwenye anga ya Dar wakati uchaguzi ni Igunga siyo Dar sijui kwanini?]. Mfano km ajali inatokea Kibaha ua Chalinze na kwa sababu foleni imelaumiwa mara kwa mara kuzuia kuwafikia majeruhi haraka basi chopper itumike na inapo kwenda kwenye tukio iende na polisi na manesi na madaktari [paramedicines] na zana za dharura ili kusomba majeruhi kuwawaisha kwenye msaada.



Ile chopper ni mali ya watz wakiwemo hao majeruhi, sasa kwanini isiwahudumie inapotokea ajali? Wakati ng'ombe [mali binafsi] wa Tryphone Maji walipoibiwa mkoa wa Pwani, chopper hii ilikesha angani mfululizo kwa wiki nzima ikitafuta wezi hao, sasa iweje majeruhi binadamau ambao kati yao wamo wataalamu wanaotegemewa na taifa???!!!!



Utaratibu wa bima urekebishwe, ili uwe na meno makali ili wamiliki wa mabasi waogope, hapa unaweza ukaletwa sheria ya kuwa kwa kuwa wamiliki wa vyombo vya usafiri wanatengeneza faida basi wawajibike kulipa fidia kwa majeruhi na wafu kwa kiwango kitachoamuliwa mbali na malipo ya bima, nia ikiwa ni kuepusha ajali za kutengeneza ili kupata faida. Tuachane na viini macho vya speed governor na utaratibu wa mabasi kusafiri mchana, mbona Kenya mabasi yanasafiri usiku miaka yote?



Kuwe na utaratibu wa maaskari kusindikiza vyombo wakisaidiana na maafisa EWURA na SUMATRA toka mkoa hata mkoa hivyo hivyo mpaka chombo kifike kinapokwenda. Maaskari na maofisa wa EWURA na SUMATRA wakati umefika wa wao kuachana na kukaa maofisini wakati watu wanapoteza maisha, e.g. ukienda maeneo mengi ya makutano ya barabara utakuta matrafik wako bize asubuhi na jioni tu, mchana utawakuta wako chini ya miarobaini wakichat sms na kusoma udaku tu wakati huko mabarabarani kwenda mikoani kuna uvunjifu mwingi wa sheria za barabara.

Majalwa.

nimesoma mawazo yako ni mazuri sana lakini je tutaanzaje? asilimia kubwa ya wenye vyombo vya usafiri ni watoto wa mama mdogo watakubali na wengine ni wafuasi wa vyama vya siri kama freemason n.k nao watakubali. tafakali chukua hatua
 
Martin S. Malecela
 
Sawa kabisa, umeleta hoja nzr sana. Ni kuwa wakubali wakatae hapo ndy sasa mbivu na mbichi itajulikana, watajulikana hadharani kwa umma mzm na huenda sasa maombi yatakuwa yamepata target badala ya sasa ambapo tunaomba jumla jumla bila kumjua mchawi ni nani? Naamini wataogopa kujulikana kwa umma. Lkn pia Malecela tujuwe kuwa ROHO wa MUNGU HASHINDWI KITU ukimkabidhi.
 
Majalwa


Hakuna maoni: