Jumatano, 5 Oktoba 2011

AJALI ZINAUWA WATU WENGI HILI NI PEPO

                 Shalom watu wa Mungu ni matumaini yangu kuwa wote ni wazima. Hii ni wiki ya nenda kwa usalama kama wanavyoiita wenyewe na sijui kama kweli watu wanaenda kwa usalama!. Wiki nimepata kusikia takwimu za ajali sehemu mbalimbali na nikagundua kuwa yamkini ndiyo kitu kikubwa kinacho sababisha vifo vya nguvu kazi ya Taifa kuliko hata Maleria na ukimwi na si hivyo tu bali inasababisha hasara kwa miundo mbinu na mali za wahanga wa ajali tena inaongeza ulemavu kwa watu kuliko hata polio. Ukisikiliza takwimu utasikia tunapoteza maelfu ya watu kwa mwaka.


                 Na sijajua kama kweli hatua zinazostahili zinachukuliwa maana inaonyesha ajali nyingi zinasababishwa na uzembe wa waendesha vyombo hivyo. Na nilichogundua kuwa wamiliki wengi wa vyombo hivi ajali haziwaathiri maana kama basi litapata ajari na lina bima basi baada ya muda anarudishiwa gari linguine tena jipya kuna kipindi niliwahi kusikia kua hata wakati mwingine wanafanya makusudi akiona gari limechakaa analipatisha ajali makusudi ili alipwe basi jipya. Lakini watu wanaopoteza uhai au viungo vyao na kupoteza mali zao sijawahi kusikia wanalipwa fidia hapa ndipo naona kuwa bima haina maana kwani badala ya kujali watu kunajali vyombo vya usafiri na sijajua lini watu watalipwa angalau kifuta jasho cha machungu baada ya ajali bali huishia kutibiwa tu na waliopoteza maisha huishia kwa ndugu zao kuwachukua na kwenda kuwazika.

                 Lakini tuangalie kwa jicho la pili hapa ninachogundua shetani anakatisha maisha ya watu wasio na hatia ili tu wasiifikie ile toba ya kweli ya kumkiri Yesu kuwa ni Bwana na mwokozi wao nimepata kusikia mara nyingi kuwa ajali nyingi zinasababishwa na wachawi, tukianzia ajali mbaya yam v Bukoba teyari wako watu ambao walishasema kuwa walisababisha enzi hizo wakiwa bado wachawi na hata ile ya tren iliyotokea Dodoma na nyingine nyingi na hata hii iliyotekea hivi karibu kule Zanzibari.na kama Biblia inavyo sema kuwa Mungu hapendezwi na vifo vya wenye dhali bali wote anataka waifikie ile toba. Hivyo ajali nyingi zinahusishwa na imani za kishirikina kutoa makafala n.k ninaamini kama mambo hayo yasingekuwepo tungekuwa tunasikia ajali mara moja kwa mwaka na si kama iliyo leo.

                   Nimalizwe kwa kutoa changamoto kwa vikundi vya wana maombi na watu tunaomwamini Mungu hebu tusimame tukapate kuipinga hili pepo la ajali linalopoteza watu wengi ninaamini inawezekana maana tumepewa mamlaka ya kufunga duniani na mbinguni na kufungulia duniani na mbinguni, ni sisi tu kuamua ili hao watu wasife dhambini . kwa utafiti wangu mdogo sio kwamba katika ajali wapendwa hawamo wamo lakini Mungu huwa anawaponya kwa namna ya ajabu sana kama kwenye ajali ya Dodoma walikusudiwa wapendwa lakini behewa walimokuwamo wapendwa hakudhulika hata mtu mmoja na wakati mwingine shetani anaweza kuua hata watu 1000 wenye dhambi kwa kumtafuta mpendwa mmoja tu. Lakini Mungu wetu ni mwema ambaye hutulinda na mabaya yote. Tuzipinge nguvu za shetani naye atatukimbia muwe na wiki njema ya usalama barabarani. chao


Ajali mbaya ya Treni Dodoma


Ajali mbaya ya gali lilokuwa limewabeba wanamziki wa taarabu


Ajali mbaya ya MV Bukoba


Hakuna maoni: