Jumanne, 4 Oktoba 2011

GRECE NYONI AJIPATIA SH 500,000/= KWA KUSHINDA SHINDANO LA KUSOMA BIBLIA




Ilikuwa ni furaha na shwangwe kwa kanisa baada mshiriki wa shindano la kusoma Biblia Grace kujihakikishia ushindi kwa kujibu maswali yote 10 aliyoulizwa. Fainali hizo za shindano la Biblia zilifanyika katika kilele cha sikukuu ya vijana katika kanisa la TAG Magomeni. Shindano hilo ambalo hushindaniwa kila mwaka lakini kwa mwaka huu limekuwa la tofauti na mvuto mkubwa baada ya zawadi za washindi kuwa kubwa. Fainali ya shindano hilo lilijumuisha vijana 10 walipata marks za juu na walipewa kila moja sehemu za kusoma na kuulizwa maswali ya papo kwa papo. Mshindi wa kwanza alikuwa Grace Nyoni aliyejinyakulia kitita cha sh 500,000/= Ushindi wa pili ulichukuliwa kijana mdogo Dennis aliyejinyakulia sh 250,000/= na ushindi wa tatu ulichukuliwa na John ambaye alijinyaKulia kitita cha sh 150,000/= na washiriki wengine 7 walijipatia sh 10,000/= kama kifuta jasho. katika shindano hilo mshiriki mmoja alikosekana baada ya kuwa amesafiri na ndipo muongoza shindano ndugu Lumelezi alipohitaji mtu yeyote aliyeyeyote aliye tayari tayari ajitokeze kanisa zima lilikaa kimya kuona ni nani atajitokeza na ndipo Tony alijitokeza na kujibu maswali 4 kati 10 na kupata sh 10.000/= ya kushiriki. Shindano hilo ambalo lilidhaminiwa na ndugu Lumelezi limekuwa ni chachu ya kuwafanya vijana wasome Biblia zao. Yeye amekuwa na kiu ya kuona shindano shindano kama hilo likishirikisha watu wengi na ibidi makanisa mengi ili watu wawe na wamko wa kusoma Biblia zao.

Grace akijibu Maswali
  
 
Grace Nyoni akiwa amebebwa juu baada ya kutangazwa kuwa ni mshindi.


Peace Lumelezi akiuliza maswali ambaye pia ni mdhamini wa shindano.
 
Tony MC Lamecky akipokea zawadi hakuwa mshiki rasmi alijitokeza hapo hapo na kujibu maswali 4 kati ya 10

  
<> 
Grace akitokwa na machozi ya furaha baada ya kutwaa kitita cha sh 500,000/=

Picha ya washiriki wote wa shindano na viongozi wa kanisa na uongozi wa vijana


Hakuna maoni: