Alhamisi, 15 Septemba 2011

NJIA ANAZOTUMIA SHETANI KUWATAWALA WATU 3


   Namshukuru Mungu kwa wema wake siku hadi siku leo nataka kuendelea na mada yetu ya kutambua mitego ya shetani nia ya mada hii iwe ni changamoto kwetu katika maisha ya kila siku tunayoishi na itusaidie kutambua hiyo mitego na namna ya kuepukana nayo tumepewa mamlaka ya kupinga kazi za shetani, hivyo kikubwa ni kusimama imara katika wokovu na tutakuwa salama maana tupo chini ya mwamba usiotikisika ambao ni Yesu kristo

   Kuna kisa nataka nikizungumzie ambacho ni cha kweli nacho kina wahusu wachawi zamani wachawi walikuwa wanarithisha familia zao huo uchawi yaani kama baba au mama ni mchawi basi anaangalia kati ya watoto wake nani awe mchawi na atamfundisha na kuendeleza uchawi katika familia yao lakini pamoja na hilo ujue kuna mtoto atatolewa kafala ili kuthibitisha kuwa wanampenda huyo mungu wao ikumbukwe kuwa shetani sikuzote anaiga mambo ya Mungu na kuyafanya kama yake sadaka, zaka, karama kama za unabii, uonaji nk hivyo vitu anavitumia tena ndivyo sivyo hakuna sadaka ya kumtoa mtu afe isipokuwa moja tu ya Yesu kristo lakini kwa shetani kafala zote ni watu na hata ajari nyingi zinazotokea ni kafala wanazotoa na hasa mwezi huu wa 9 na 12 kama una kumbu kumbu nzuri mpaka sasa kuna ajari nyingi zimeshatokea tena sio Tanzania tu bali sehemu mbali mbali Duniani pamoja na kwamba kuwa nchi nyingine zinatamani kufanya dunia kuwa ni mahali salama lakini hilo ni ngumu amani na usalama wa kweli unatoka kwa Mungu. Kuna makundi mengi ya sili yanayofanya kazi mchana na usiku kuhakikisha watu wanakufa bila hatia.
   Katika siku za leo wachawi wamebadilisha mfumo na wanachofanya ili kuwa na wachawi wengi, ni kila mchawi katika eneo lake kukusanya watoto wakati wa usiku kiuchawi bila wazazi kujua na kuwa fundisha uchawi na kwasababu ni watoto wanakuwa waaminifu kutunza siri za makundi hayo. Ni mtoto wa mama yangu mdogo alikubwa na tukio kama hilo kuna mama jirani yetu alikuwa anawakusanya usiku na kuwafundisha uchawi na kwenda nao kwenye mambo yao na ilichukuwa mda mrefu mpaka kugundua jambo hilo ni baada ya kuwa matokeo mabaya shuleni walimu wakawa wanamwazibu kila siku na akwana mtindo wakusinzia darasani kutokana na adhabu alichoka na siku moja akiwa nyumbani wakati wa usiku alisikika akigoma kundoka nyumbani baada ya kuja kuchukuliwa na Yule mchawi na hakuwa anaonekana ila yeye alikuwa akimwona na kusikia sauti yake anavyo mwita usiku huohuo ndiyo akaletwa nyumbani na kufanyiwa maombi na kueleza aliyokuwa akiyafanya usiku na ndiyo ukawa mwisho wake wa kufundiswa uchawi. Hivyo basi sasa hivyi wachawi wanatumia njia hiyo tunatakiwa kuwa makini kufuatilia nyendo za watoto wetu na kuwaombea sana na kuwafunika na damu ya Yesu ili mambo kama hayo yasiwapate maana hata pata nimesikia kesi nyingi kama hizo na ndo maana siku hizi utakuta watoto wengi wakifanyiwa maombi wanpagawa sana na pepo hizo ni roho zinazopandikizwa ndani ya watoto kutoka kwa shetani na akijua kuwa watoto hao wakiachiwa wajue mambo ya Mungu mbele ya safari watakuwa jeshi kubwa ambalo litamsumbua yeye mwenyewe hivyo yeye anacho fanya ni kuwahi mapema kabla wapendwa wengi hawajajua mbinu hiyo. Na wewe kama ni mwalimu wa watoto iwe kanisani au popote hebu Mungu akutumie ili kizazi cha watoto wa Mungu kiongezeke na tunatakiwa tumtake Mungu na nguvu zake ili adui asipate nafasi katika familia zetu na yeye shetani siku zote ni kupotosha tu ukweli wa mambo ya Mungu na ndo maana hata watoto wa wachungaji wanakuwa na vita kubwa katika makuzi yao na wengine wanakuwa hawana maadili mazuri wa hata kutokuata nyendo za wazazi wao (wachungaji) hiyo inatokea ili wasiomjua Mungu waone kuwa wokovu au kufuata Mungu ni usanii.

   Wakati tulio nao ni wakutafuta Mungu sana kama tunataka kupona lakini kama tunataka kuangamia basi tuendelee kuwa na maisha ya kawaida katika wokowu. Na kufuata mkumbo wa dunia badala ya kufuata neon la Mungu linasema nini na neon hilo ndilo liwe mwanga wa njia zetu usiongozwe na akili zako maana amelaaniwa amtegemeaye mwanadamu bali uongozwe na Roho mtakatifu. Amen

INAENDELEA
Chapisha Maoni