Jumatatu, 12 Septemba 2011

ADUI NA MATATIZO TUNAYOKUTANA NAYO YAWE NI CHANGAMOTO YA KUSONGA MBELE.

Kila jambo tunalifanya linakuwa na vikwazo na vikwazo huwa vinategemea hilo jambo ni kubwa kiasi gani kama jambo lenyewe ni kubwa sana na vikwazo vyake vitakuwa ni vikubwa na kama jambo lenyewe ni dogo basin a vikwazo vyake ni vidogo. Mara nyingi watu wengi tumekuwa ni wpesi wa kukata tama tunapokutana na mambo magumu na mara nyingine hatutaki hata akili zetu kujishugulisha na mambo hayo magumu na wakati mwingine hata kumchukia Yule anayesababisha hayo mambo magumu na kufanya kuwa adui inaweza kuwa boss wako ndugu yako n.k. lakini leo nataka ujue kuwa adui zetu na matatizo tunayokutananayo katika maisha yetu yasiwe vikwazo vya kukata tama na kurudi nyuma bali iwe ni ngazi ya kufikia mafanikio.Unakuwa na tatizo au kikwazo katika mambo yako uiangalie kile kikwazo angalia faida utakayopata baada ya kuvuka kikwazo! Glory to God najua hujanipata. Nitafafanua kama utaangalia kikwazo ulicho nacho kweli utakata tamaa maana ni kikubwa lakini kikwazo kimewekwa ili ikikwazue na jaribu limeletwa ili ulishinde changamoto zipo ili tujifuinze na kusonga mbele ni sawa na mwanafunzi haiwezekani kila siku akasoma bila kupewa test au mitihani na kama wewe unakimbia test na mitihani basi wewe si mwanafunzi. Ukisoma 1Sam 17:26 inamuonyosha Daudi baada ya kuwa na tatizo katika Taifa la Israel la kutukanwa Daudi aliuliza atafanyiwa nini atakaye muua Goliati alipopewa jibu Daudi hakuona tena ukubwa wa Goliati bali yeye aliangalia faida atakazozipata baada ya kupiga Goliati na kweli akampiga. Hata kristo katika ubinadamu aliokuwa nao alitamani kikombe kimuepuke maana mateso ya msalaba hayakuwa mchezo lakini aliangalia baada ya kuvuka hapo kuna nini mbele yake hivyo ikamsaidia kuvumilia mateso makali ya msalaba.


Siku zote wafanye adui zako na vikwazo vyako kuwa ni stepping stone ya kusonga mbele na si vizuizi. Fikiri kana Hanna bila Penina kumcheka na kumsema kila wakati Hanna asingepata uchungu wa kumwomba Mungu ili ampe mtoto inaweza kuwa Hanna alimuona kuwa Penina ni adui yake lakini mimi niseme ndiye aliyemsaidi sana Hana kupata mtoto na ninafikiri kuwa kama Penina asingekuwepo sidhani kama Hana angepata mtoto. Hali kadhalika Daudi bila Goliati isingejulikana nguvu ya Mungu iliyokuwa ndani ya Daudi, Wana Israel Bila wa Misri Mungu asingeonyesha miujiza mikubwa kama aliyo tenda, Elia bila Manabii wa baali muijiza wa kushusha moto usinge tokea.


Nafikiri ndugu wapendwa mmenipata usizikimbie zangamoto kabiliana nazo ukizikimbia leo utakutana nazo siku nyingine dawa ya mtihani ni kuufanya sio kuukwepa maana utakutana nao tu huwezi kwenda sekondari bila kufanya mtihani wa darasa la saba na huwezi kwenda chuo kama hujafanya mtihani wa sekondari . barikiwa sana.

Hakuna maoni: