Jumatano, 20 Julai 2011

TABORA YAVAMIWA!!! WACHAWI 2 WANASWA.


Timu ya uinjilisti kutoka Dar es salaam (All Nations Christian Centre) TAG Magomeni  imevamia mji wa Tabora na vitongoji  vyake niliongea na mwinjilisti  Kazimoto ambaye yeye ni mhubiri katika mikutano yote miwili. mmoja ambao ullifanyika Urambo katika kitongiji cha Usoke amesema mkutano ulikuwa ni mzuri na nguvu za Mungu zimeonekana sana na watu wapatao 46 wameokoka na wameanza semina ya kukulia wokovu na wengine wengi kufunguliwa kutoka katika vifungo ya shetani.  Msafala huo ambao unaongozwa na mwenyekiti ndugu Enocky kipwate, Wanaendelea na mkutano mwingine ambao unaendelea, unafanyika Tabora mjini kwenye kanisa la mtume Cyprian Lijongwa ambao ni wa siku 8 ulioanza tar 17/07 utaendelea hadi tar 24/07/2010 ambao una wahubiri watatu ambao ni mch  Raul kutoka Amerika, mwinjilisti Kazimoto ambaye anaanza leo na atamalizia mch Steven wote hawa ni mazao ya Magomeni TAG. Akiongea kwa njia ya simu Mama John Nyerere alinijuza mwandishi wa habari hii kuwa Mungu ameonekana sana katika siku 3 za mkutano ambazo alihubiri mch kutoka Amerika na jana Jumanne kuna wachawi  walinaswa na nguvu za Mungu katika eneo la mkutano haikujulikana mara moja kuwa wachawi hao walifika mkutanoni kufanaya nini waliombewa na kumpokea Yesu. Alimalizia na kuomba maombi kwa kanisa ili Mungu aonekane zaidi ili watu wafunguliwe na kupokea Yesu kama Bwana na mwokozi wa maisha yao. Haya kila aliyesoma ujumbe huu hebu ombea Mungu akaonekane huko Tabora na upako wake ukawe juu ya watumishi walioenda kwenye hiyo huduma akawatumie kwa namna ya kipee na zaidi ya yote jina la Yesu likainuliwe juu zaidi. Jina la Bwana libarikiwe.

Hakuna maoni: