Jumatano, 20 Julai 2011

KUWATUMIKIA WENGINE NI KUMTUMIKIA MUNGU

Unawezaje kusema unampenda Mungu usiye mwona na huku unamchukia ndugu yako unaye mwona? Haya ni maneno aliyoema bwana Yesu. Maisha ya bwana Yesu alipokuwa Duniani kitu kikubwa alichokionyosha kwa wanadamu ni upendo. Hicho ndicho kitu kikubwa ambacho karibu asilimia kubwa alifundisha na kutoa mifano mingi ambayo nikisema niorodheshe hapa utasoma mpaka utachoka. Nianze kukupa maandiko tuanze Luka 10:30 inayozungumzia habari za msamalia mwema hapa kidogo kuna changamoto kwa habari ya kuwatumikia wengine. Tunaona kwa katika jambo hili haijalishi kuwa wewe una cheo gani kanisani unaweza ukawa kuhani lakini uka feli kwenye hili la kuwatumikia wengine. kwa Yesu alimtaja kuhani na mlawi ambao enzi hizo walionekana wanaijua dini ya kiyahudi vizuri hii inamaanisha kuwa unaweza kujiona una haki mbele za Mungu kumbe kuna mambo mengine ambayo yanakushinda na ndiyo maana ni vyema kumwomba Roho mt akuchunguze na kukurekesha pale tunapoenda ndivyo sivyo kama kuna njia yoyote iliyombaya akufanye vile apendavyo. Nikirudi kwenye mada yangu tunaona msamalia anapongezwa na Yesu kwa kufanya vizuri ijapo kabila la wasamalia ni kati ya makabila yaliyokuwa yanadharauliwa kipindi hicho. Tabia za Mungu ni upendo tena upendo wa agape ambao hauna kikomo na ukisoma 1 wakor 13 sura yote inazungunzia upendo na ikichunguza sana unaweza kuona watu wengi hatuna upendo huu unaozungunziwa kwenye sura hii, upendo wetu bado unakuwa na dosari Fulani Fulani hivi.Kwanini nimezungumzia upendo hapa usije ukadhani nimetoka nje ya mada hasha mimi ninachoamini huwezi ukawatumikia wengine kama huna upendo tena upendo wa kimungu kama hutakuwa nao basi utatumika kwa maslahi Fulani au kwa muda halafu utaacha lakini kama utakuwa na upendo wa Mungu unaozungumziwa kwenye wakor 13 mi nakwambia hutaacha kuwatumikia wengine maana utasikia hatia moyoni mwako. Lakini kwanini nyakati tulizo nazo ni ngumu kuwatumikia wengine?! ni kwasababu tumeshindwa kuachilia mioyo yetu itawaliwe na pendo la Mungu, upendo tulionao ni ule wa kawaida tu ambao hubagua,una majivuno, una fitina, una kutokuwa na adabu, una chuki nk. Na katika siku za leo hata wapendwa nao wanachukiana, wananuniana, kunakuwa na magomvi n.k sasa je? Kama tunamchukia jirani yetu tunayemwona tunaweza kumpenda Mungu tusiyemwona. Jibu unalo.


Tuangalie mstari mwingine Math 25:34 – 44 naomba uusome kwa makini hapa Yesu anaelezea kwamba tunatakiwa tuwatumikie wengine kwamba alikuwa mgonjwa akahudumiwa, alikuwa na kiu akanyweshwa, alikuwa uchi akavishwa, n.k hapa inaonyesha kuwa Yesu anakuwa ndani ya wahitaji tunapowapa mahitaji wahitaji basi hili linambariki Mungu sana atamuonea fahari mtu huyo kwa tendo lake hilo na linaweka kumbukumbu hata katika ufalme wa Mungu msitari wa 40 Na mfalme atajibu akiwaambia, amini, nawambia, kadiri mlivyomtendea mmojawapo wa hao ndungu zangu walio wadogo, mlinitendea mimi. Hapa moja kwa moja inaonyesha kuwa tunatakiwa tuwatumikie wengine tena wale wahitaji tofauti na siku hizi tunapenda kuwatumikia watu wenye uwezo wenzetu na si wahitaji. Wahitaji ni wengi wanaotuzunguka tena watofautiana uhitaji wao huwezi ukasema kuwa huna cha kuwapa viko vitu vingi vya kutoa kuwasaidia kuna kuwatembelea wagonjwa mahospitalini, magerezani, mashuleni n.k


Nimalizie na Mith 19:17 ambao unasema Amhurumiae maskini humkopesha Bwana naye atamlipa kwa tendo lake jema, Maskini hapa ni yeyote mwenye uhitaji na hapa hutakiwi kuhoji kuwa unayempa ni dini gani au kabila gani hii ni amri wewe fanya ili umkopeshe Bwana sasa kama unataka umkopeshe Mungu basi Watumikie wengine onyesha upendo,fadhili, furaha nk. Kuna siku moja kuna mtu mmoja alienda kanisa fulani kuomba msaada alipofika katika kanisa hilo alifukuzwa kwa kutoa sababu kuwa huko nyuma aliwahi kuja mtu kama yeye akawatapeli hivyo hawatoi msaada kwa mtu yeyote mwenye shida kama yake. Kwa upande wangu naona hii si sawa wewe kinachotakiwa ni kumhudumia mhitaji hata wakija kila siku wewe hudumia tu Mungu hakutoa idadi kuwa tuhudumie kadha hapana, labda usiwe na cha kumpa lakini kama kipo we toa tu maadamu uwezo unaruhusu Mungu atatulipa kwa tendo hilo jema. ijapo watu tunapenda kukopeshana sisi kwa sisi lakini sasa jaribu kumkopesha Bwana maana hata neno lake linasema tumjaribu tuone kama hatafungulia Baraka hata kusiwepo mahari pa kuweka.!!!! hivyo basi tupende kuwatumikia wengine maana kumtumikia mwingine ni kumtumikia Mungu. Chao.


Chapisha Maoni