Shalom,
Tunamshukuru sana Mungu kwa jinsi ambavyo anaendelea kuonekana katika mkutano wetu ambapo watu wanaponywa na kuokolewa. Wachawi wamekutana na nguvu za Mungu na watu waliolishwa sumu wamekutana na nguvu za Mungu za uponyaji.
Idadi ya wanao-okoka pia imeenda ikikua kila siku na kesho j2 tunatumai kuwa na umati mkubwa wa watu katika mkutano huu.
Wamama nao hawajabaki nyuma wako kumpokea Bwana Yesu awe Bwana wa maisha yao |
Watoto nao wako mstari wa mbele kuona kila kinachopendelea. |
Watoto wamejipanga ili kuiongozwa sara ya toba. |
Mikono juu kumpokea Bwana Yesu. |
mmojawapo ya wahubiri wa mkutano Mwinj Kazimoto akiweka mikono juu ya wenye matatizo. |
Wamemakinika kufuatilia kila kinachoendelea katika mkutano. |
Hata wabibi nao hawakuwa nyuma na hawajachelewa kumpokea Yesu wakiongozwa sala ya toba. |
Timu ya wana Magomeni wakipata kifungua kinywa kwa furaha za ushindi katika jina la Yesu. |
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni