Jumatano, 1 Juni 2011

UMEMKUMBUSHA BWANA AHADI ZAKO ISAYA 43:26.

 Ahadi za Mungu siku zote zipo kwaajiri yetu. Mungu alipotuumba aliumba mazingira yenye utoshelevu wa mahitaji yetu ya kila siku, na mpango wa Mungu haukuwa mwanadamu aumbiwe shida, yaani hatukuubwa tupate shida bali alituumbia maisha yenye raha msarehe na tutawale vitu vyote vinavyoonekana na visivyoonekana.Mwa 1:27- 29 kusudi la Mungu ni sisi kutawala na si kutawaliwa. Mambo yaligeuka tu pale Adamu na mkewe walipokula tunda la mti waliokatazwa Mwa 3:16. Ashukuruliwe Mungu kwa upendo wake kwa kumtoa Mwanae wa pekee Yesu ili kuja kutuokoa na kuturudishia mamlaka (utawala) Yoh 3:16. Hivyo sisi tulio okoka tunarithi Baraka za Ibrahim kwa imani na kwa damu ya Yesu iliyotupatanisha kwahiyo zile Baraka ambazo tulinyang’anywa hapo mwanzo zinarudishwa kwa kifo cha Bwana Yesu pale msalabani. Hata sasa tunatakiwa kutawala na si kutawaliwa. haki zetu au Baraka zetu ni sawa na matunda yaliyoiva yaliyo juu ya mti ambayo yanasubiri mtu mwenye shabaha kuyaangua tu hayo matunda hebu soma habari za kaka yake na mwana mpotevu. Luk 15:29- Yule kaka yake na mwana mpotevu ambaye alikuwa na haki ya kutumia vitu vya baba yake lakini hakuitumia japo ilikuwa yake. kwasababu hakudai au hakumwomba baba. mdogo wake alipopatikana na kuchinjiwa ndama yeye akalalamika kana kwamba baba yake hampendi lakini kumbe sivyo. Jibu la baba yake lilikuwa zuri sana alisema mwanangu wewe u pamoja name siku zote na vyote nilivyo navyo ni vyako!!!!!! Tena kufanya furaha na shangwe ilipasa. Ikiangalia hapa utagungua kosa lilikuwa la mototo na si la baba ni yeye mwenyewe hakutambua kuwa alitakiwa ajipe raha mwenyewe. Hata siku za leo kuna ahadi nyingi sana ambazo Mungu ametuahidia lakini hatumkumbushi, na kutomkumbusha kunasababisha kutokutimizwa kwa ahadi za Mungu na kosa hapa si la Mungu ila ni sisi ambao hatumkumbushi Mungu kutimiza ahadi zake. Na hii imekuwa ni tatizo kubwa kiasi kwamba watu wamedhani kuwa Mungu hatendi kitu katika maisha yetu ni kama amewaacha wanadamu kama yatima au kama kondoo wasio na mchungaji lakini sivyo a hadi za Bwana zipo na wanao zidai wanapewa na wewe usipozidai shauri yako. Bwana anasubiri tu peleke hoja zenye nguvu zitakazomshawishi Bwana kufanya Isa 41:21 . wewe hoja zako zenye nguvu ni zipi? Sasa basi mweleze Mungu Atakufanyia yeye anasema hakuna jambo lolote gumu asilolieza. Yer 32:27Nataka tukumbushane baadhi ya ahadi


1. Bwana atakufanya kuwa kicha na wala si mkia Kum 28:13


2. Bwana atabariki kazi za mikono yako nawe utakopesha mataifa mengi wala hutakopa wewe Kum 28:12


3. Bwana ndiye mchungaji wangu sitapungukiwa na kitu Zab 23:1


4. Atawatiisha watu wa nchi chini yetu Zab 47:3


5. Ukaniite siku ya mateso nitakuokoa na wewe utanitukuza Zab 50:15


6. Akusamehe maovu yako yote akuponya magonjwa yako yote Zab 103: 3


7. Usiogope Isa 43:1b – 4


8. Na kwa kupigwa kwake sisi tumepona Isa 53:5


9. Angalia nimekuweka leo juu ya mataifa na juu ya falme ili kung’oa na kubomoa…..Yer 1:10


10. Niite nami nitakwitikia Yer 33:3


Zipo ahadi nyingi sana ambazo tunaweza kumdai Bwana na akafanya maana neno linasema Mungu si mwanadamu hata aseme uwongo. Na yeye huliangalia neno lake ili aweze kulitimiza. Mimi naamini kama tukisimama katika zamu zetu na kumkumbusha Mungu ahadi zake katika maisha yetu, hatutakuwa si watu wa kawaida kabisa maana tutabarikiwa mpaka basi, tutaponywa magonjwa, tutakuwa na ulinzi katika familia zetu,tutakuwa vichwa na si mkia, tutajua mambo makubwa na magumu mpaka watu watushangae, tutakuwa Baraka kama Baraka za Ibrahimu ambaye tunatakiwa tujifananishe naye. Watuhawatapungua katika nyumba zetu kwa kufuata wema wa bwana. Ni maombi yangu Roho mt akusaidie kuelewa nenolake , ubarikiwe sana na tuonane wakati mwingine.


Chapisha Maoni