Jumatatu, 16 Mei 2011

JE OSAMA BIN LADENI ALIKUWA GAIDI KWELI?


 Marehemu Shekhe Osama Bin Laden aliyekuwa kiongozi wa kundi la Al-qaeda.


  Shalom ndugu wasomaji wa blog yangu ni matumaini yangu ni wazima kwa neema za Mungu wetu aliye hai. Ni wiki mmoja imepita tangu kutangazwa upya kwa habari ya kifo cha Osama bin Ladeni. Nasema kutangazwa upya maana ilisha wahi kutangazwa mwaka 2001 kuwa Osama alikufa kwenye mahadaki ya torabora huko Afrighanstan baada ya majeshi ya Marekani kushambulia mapango hayo kwa makombola mazito yaliyo vunja vunja miamba ya mapango hayo na habari zake zikaishia hapo. Wengi, mmoja wapo mimi niliamini habari hizo kuwa Osama Alisha kufa kitambo. Kabla sijaeleza kama yeye ni gaidi au laa hebu tupate historia yake. kwa ufupi yeye ni mzaliwa ya Saud Arabia katika familia ya kitajiri na alikuwa katika malezi ya kiislam kwani amezaliwa katika familia ya kiislam na nchi ya kiislam na alisoma mpaka chuo kikuu na haikuishia hapo alipata nafasi ya kwenda kusoma Marekani, pia aliwahi someshwa na serikali ya Marekani kwenye shirika lao la kijasusi CIA na lengo la Marekani ilikuwa imutumie Osama katika vita Baridi iliyokuwa ikiendelea na USSR Jamhuri ya Warusi na kipindi hicho Osama alikuwa ni rafiki mkubwa sana na Marekani na alifanya kazi hiyo na baadae kuwageukia wamarekani baada ya kuona sera zao zina lengo la kuagamiza dini ya mama mdogo. kwa kweli kikulacho ki nguoni mwako na mtoto wa nyoka ni nyoka, Marekani hakujua kuwa ipo siku moja Osama atageuka na kuwa mwiba kwao na kama wangejua wasinge msomesha. Kwanza alianza vizuri kwa kuwa wakala mwaminifu lakini siku zilivyozidi alibadilika kutokana na sera za Marekani za kutopatana na sera za nchi za mama mdogo, sasa kwa kuwa Osama alikuwa nyoka akaona ni vema abaki kuwa nyoka na kuwa kinyumbe na Marekani na kwa kweli alisumbua sana kwa kuwa alikuwa anajua mengi kuhusu Marekani na aliyofundishwa katika shirika la kijasusi la Marekani. Baada ya kujua kuwa marekani siku zote sera zake zinagandamiza sera za watoto wa mama mdogo, kwa upendo uleule uliokuwa mkubwa ukageuka na kuwa chuki kubwa na kuanza mipango ya kuanzisha kundi la al-qaeda iliyosababisha maafa na ulemavu kwa watu wengi wasio na hatia likiwa na lengo la kuleta heshima kwa mataifa ya mama mdogo. Katika kila jambo huwa kuna ubaya na uzuri wake na hayo yote yatapimwa kutokana na ufahamu wa mtu mwenyewe. wewe wakati unasema pombe ni mbaya mwingine anasema kuwa ni nzuri na hata acha. Na kwa upande wa Osama ambaye anaungwa mkongo na watoto wa mama mdogo kwa asilimia kubwa hata hapa nchini, kwa uchunguzi nilioufanya.alikuwa sahihi asilimia 100 kwa yale aliyokuwa anayafanya ambayo kwa upande mwingine yanaitwa ni ya kigaidi.

Shekhe Osama Bin Laden alikuwa gaidi?
Jibu lake lipo katika pande mbili wako waliomuona ni gaidi ambae anastahili kuuliwa popote atakapo onekana, lakini walikuwepo waliomuunga mkono na kumuona ni mtu safi anayetimiza utetezi juu ya dini ya alah. Katika uchunguzi nilioufanya nimegundua kuwa waislamu wengi wanamkubali sana Osama na maana nyingine kwao wao sio Gaidi na hata Al-qaeda katika walaka wao walioutoa wamesema wamempoteza mtetezi wa waislamu na kiongozi shupavu ambae siku zote alisimama kidete kuwatetea kutoka kwa uonevu wan chi za magharibi ambazo ndizo zina wakristo wengi. Pamoja na familia yake watoto na wajukuu najua ukiwauliza hawawezi kusema kuwa baba yao alikuwa gaidi zaidi ya kusema alikuwa mtetezi wa dini ya mnyazi Mungu na kufa kwake kunaonyesha ameifia dini. Hata ikifuatilia vyombo vya habari va kiislamu utaona hilo pamoja na waislamu wengi niliohojiana nao wale wenye msimamo mkali hawasemi kuwa si gaidi bali ni mtetezi wao dhidi ya sera za kibabe za marekani. Ukija pande wa pili wawakristo anaonekana alikuwa gaidi kutokana na kusababisha mauaji yasiyo na hatia na kuna sera iliyoanzishwa katika uongozi wake wa kuwaingizia imani na itikadi kali sana hata kufikia hatua ya mtu kujitoa mhanga na kuitwa mfia dini. Na mbinu hii diyo inayotumika sasa katika sehemu mbalimbali hata mauaji yaliyotokea huko Pakstani ambako watu zaidi ya 80 wamekufa na wengi kujeruhiwa na wao al-qaeda kuthibitisha kuwa wao wamehusika ni ya kujitoa mhanga. Hivyo basi hizo ndizo pande mbili za Osama bin Laden kuwa ni gaidi alistahili alichofanyiwa na wengine kusema sio gaidi ni mtetezi wadini ya mnyazi mungu na ninajua kwa maelezo haya uakuwa na msimamo wako mwenyewe na kuwa katika upande moja wapo kati ya hizo mbili. Ili imethibitika kuwa ameuwawa na makomandoo ya kimarekani waliovamia nyumba yake aliyokuwa akiishi huko Pakstani na kuzikwa baharini na kuoonyeshwa kwa picha za mazishi yake kwa kile kilicho elezwa na Marekani kuwa kitachoche hasira kwa watoto wa wa mama mdogo. Ubarikiwe sana tukutane wakati mwingine.

Hakuna maoni: