Jumatano, 1 Juni 2011

NJIA MBALIMBALI ANAZOTUMIA SHETANI KUWATAWALA NA KUWATUMIKISHA WATU NO 2

2. MAVAZI, VIPODOZI NA MAFUTAMavazi nayo hayako nyuma kama mwazo nilivyosema kuwa kuzimu kuna viwanda vya kila kitu ujue hata mavazi yanatoka huko tena mitindo mingi ya mavazi zinabuniwa kuzimu na zinakuwa na mvuto sana style ya mlegezo, kuva heleni na mitindo mingi ambayo kwa tamaduni zetu si nzuri hizo huanzishwa huko kuzimu na watu wengi wanavutwa nayo mitindo hiyo inakuwa na mvuto mkubwa sana, kuna mitindo ya nguo fupi ambazo kimaadili huwezi kuvaa, lakini unakuta wengine wameva tena wako comfortable tu, ujue ufahamu wake umegeuzwa vitu ambavyo si vya kawaida yeye anaona ni sawa tu ujue zindiko au dawa wanaoweka zimesha mkolea mtu huyo. siku hizi watu wazima wana vaa nguo za wadogo zao yaani nguo za kubana na wanabana maziwa yao yani ni pepo kabisa. mi sijui watu mitindo huu wanaupendea nini yaani ni aibu tupu lakini utakuta mtu mzima hana habari na si kosa lake ufahamu wake umeshapinduliwa na hata kama ukiona mpendwa kava huyo si mwezako mwombee ameshapinduliwa. Wakati mmoja kuna mchawi aliyeokoka aliniambia kuwa wakati alipokuwa mchawi walikuwa wanachukuwa mimba za wanawake (wengi anadhani kuwa mimba meharibika kumbe imechukuliwa kichawi kwaajiri ya kazi zao) na wanaenda kutengenezea mafuta ya nywele na vipodozi na kila atakayepaka tayari anaingia kwenye nila za shetani hata afanyeje hatoki labda Yesu aingilie kati aliongeza kusema kuwa hata watoto wachanga kuzimu ni dili na ndo maana watoto wengi hufa chini ya umri wa miaka 5 huku Dunia inafanya kazi ya kuzuia vifo vya watoto na mama wajawazito kumbe anayesababisha ni shetani maana kwake ni malighafi ya muhimu sana, Dunia ingejua ingefana maombi tu na si vinginevyo maana vita hivi si vya damu na nyama bali ni vya kiroho pamoja na juhudi wanazofanya hawajapunguza chochote maana hizo ni vita za rohoni na si za kimwili. Hivyo mafuta mengi ya nywele, mwili, lipstick, lip shine na vikolokolo vingine, juzijuzi nimesoma ushuhuda mmoja kwenye gazeti unaomweleze mtoto mdogo aliyejifunza uchawi na yeye kazi yake ilikuwa ni kujitahidi kugusa matumbo ya wajawazito na akisha fanya hivyo tu ujauzito huo unatoka hapo hapokwa huyo mama kusikia maumivu makali sana huo ujauzito wanenda kufanyia mambo yao ya kichawi. Hivyo vitu vingi sio salama kuwa navyo makini hakikisha unaviombea kabla hujavitumia ili visikudhuru, mimi nilifundishwa kuwa kitu chochote usikitumie kabla hujakiombea hiyo inasaidia kuondoa hila za shetani zilizoko kwenye hivyo vitu.


3. VYOMBO VYA HABARI


Ninapozungumzia vyombo ya habari namaanisha magaeti,redio,tv. Vituo vingi ni vya wamataifa hivyo hakuna jambo jema hata moja hata taarifa za habari ambazo watu tunapenda kuangalia/kusikiliza hazina faida katika ufalme wa Mungu habari hizi ni za hapa duniani tu. Vipindi vingi vinavyoweka ni vya kukupotezea muda wako mzuri na Mungu huko nako kuna mvuto wa ajabu utakuta mtu kang’ang’ania gazeti anasoma page zote, lakini mwambie asome biblia hata nusu ukrasa hamalizi!!! kwanini kule kwingine kuna mvuto au mtu ataangalia tamthilia we akitoka hapo ataangalia filamu wee nazo zinakupotezea muda tu mwambie mtu huyo aombe uone maneno mawili usingizi. Karibu asilimia 90 ya vipindi vyao zinapotosha maadili na viko upande wa shetani kabisa lugha wanazotumia miziki wanayoweka nk, maana vipindi wanavyonyesha hivyo ya nje ndiyo vinavyosababisha hata watu wavae nguo mbaya zisizo na maadili hata lugha zinazotumika ni za kihuni na karibu tamthilia zote na filamu hata hizi za kitanzania ambazo hata wengine mnazipenda zinahusu mapenzi na bahati mbaya na watoto nao wanaziangalia unafikiri wanajifunza nini hapo!!! ndiyo maana siku hizi watoto wakuna kitu wasicho kijua maana ukimkataza ataangalia hata kwa jirani. Kuna vipindi vingine vya redio ni vibaya sema sina uwezo ningekuwa na uwezo ningevifungia vote. wanaongea maneno mabaya yanayochochea ngono, na magazeti ndo kabisa usiseme hadithi zilizomo umo hazifai, picha yaani ni vurugu mtindo mmoja, ni magazeti machache sana ambayo utakuwa nao likawa na habari nzuri lakini uzuri wake ni wa hapa duniani hazina sehemu kabisa katika ufalme wa mungu zaidi tu yakuwapotezea muda wapendwa. Nilifanya tathimini nikagundua wapendwa bado tuna vituo vichache vya redio, tv na magazeti yetu yanatoka mara moja kwa juma vyote hiyo havitoshelezi mahitaji yetu na hivyo kulazimu watu kuangalia, kusikiliza na kusoma mambo mengine. upande wa tamthilia hakuna tamthilia kabisa zinazochezwa na watoto wa Mungu ukasema zinamaadili mazuri hakuna. filamu nazo hakuna ukilinganisha na zinazochezwa na wamataifa na hata wakiingiza filamu za kilokole wanapotosha ukweli wenyewe zinakuwa na mapungufu. Kingine hapa ni matangazo ya biashara yanayotolewa hasa yale ya pombe, sigara, kondomu nk, watengenezaji wake ni wataalamu na siku zote yanavutia sana na yanakuwa na mvuto kweli nayo si mazuri hasa kwa watoto wetu kutokana na upeo wao mdogo na mvuto wa matangazo yenyewe yana weza kuwashawishi kufanya vitu visivyo sahihi. Mimi nina motto mdogo wa mwaka mmoja na miezi mitatu cha kushangaza wakati wa matangazo utaona anakaza macho na kutulia na ninaamini kuna kitu kinaingia akilini mwake na mimi siwezi jua anawaza nini. Mi nakumbuka nikiwa na umri kama 11 siku moja nilienda kununua sigara na pipi kujaribu kuona vina radha gani baada ya kuona watu wakubwa wanafanya hivyo nashukuru Mungu niliishia kuonja tu na sikuendelea na tabia hiyo. lakini kuwa watoto wengi huangukia kwenye utumiaji wa pombe, sigara bangi , madawa ya kulevya, ngono, hasira, ubabe, chuki, ugomvi n.k kwa kuona na kuiga na kushindwa kuacha kabisa na hili si geni maana hata watoto wengi wa wapendwa na wachungaji wameangukia katika mtego huu omba sana na tuombe sana hi mitego ya shetani isiwanase ndugu na watoto wetu inauma sana. Hivyo ninachomaanisha hapa sio kuacha kupata habari kupitia njia hizi bali tunatakiwa kuwa wajanja kama nyoka na tukijua kuwa hatuna muda wa kupoteza tunatakiwa tuukomboe wakati na tunda la roho la kuwa na kiasi lifanye kazi ndani mwetu ili isije kukajisahau kana kwamba hapa Duniani ni kwetu.


ITAENDELEA


Chapisha Maoni