Alhamisi, 5 Mei 2011

NJIA MBALIMBALI ANAZOTUMIA SHETANI KUWATAWALA NA KUWATUMIKISHA WATUShalom ni matumaini yangu kuwa umzima kwa neema za mwenyezi Mungu. Leo nataka tupeane changamoto inaohusu njia mbalimbali ambazo sheani antumia kutawala, kutuvuruga,kukwamisha au kuturudisha nyuma katika mambo ya kimungu na kijamii . Ibilisi anafanya kazi mchana na usiku na ana njia nyingi anazotumia, na mara nyingi inakuwa ngumu hata kutambua wakati mwingine anakuja katika hali ya mwili wa kitu fulani, au anapitia kwenye kitu furani mf chakula, maji,nguo,mafuta, mawazo ilimradi tu aweze kuingia na kuleta uharibifu. kuna ushuhuda mmoja kuhusu jinni, kuwa jini linaweza kujigeuza atakavyo anaweza akawa panya akaleta uharibifu wa vitu vyako, au mende, mbu wakasababisha malaria na hela zako zikatumika katika matibabu tu bila kufanya mambo ya maana na wakati mwingine akawa mdudu n.k, ila vyovyote vile atakavyo jibadilisha lengo lake kubwa ni kuleta uharibifu katika maisha yetu na kupotosha watu wasiweze kumwabudu na kumtumikia Mungu, maana anajua muda wake hapa Duniani umebaki mchache sana, na ameshika maeneo mengi ambayo hata watu tuliokoka wakati mwingine tunajikuta tunaangukia kwenye mitego hiyo, shetani akiwa ni mtawala wa dunia hii na bahati mbaya sana sisi tuliokoka tunaisha ndani yake, yeye hutumia kila njia kwa kupitia majeshi ya pepo wabaya na wanadamu ambao ni watumishi wake kuhakikisha anaenda na watu wengi kwenye jehanamu ya moto. na si hivyo tu bali anapunguza makali wa watu wa Mungu ili afanikishe maovu yake maana kama ukiwa na nguvu za Mungu na kuomba anapata upinzani mkubwa wa kutimiza kazi zake za uharibifu, akikudhofisha nguvu ya Mungu itapungua na itonekane hakuna faida katika kumtumikia Mungu. nitajaribu kwenda hatua kwa hatua ili tuweze kufahamu mbinu zake mbalimbali anazotumia kwa msaada wa roho mtakatifu. Mara nyingi amekuwa mjanja na anabadilisha staili kila kukicha na wanakati mwingine anakuja kama malaika wa nuru kumbe sivyo. Yote hayo anatafuta namna ya kumpumbaza mwanadamu asimwabudu Mungu katika roho na kweli na kwa njia hizo anawapata wengi.

VINYWAJI NA VYAKULA

Vyakula vyote tunavyotumia viliumbwa na Mungu ili tuvitumie vilete afya na nguvu katika miili yetu ili tuweze kuishi na kufanya kazi zetu za kila siku, lakini katika siku za leo kutokana na maendeleo kuongezeka na idadi ya watu, vyakula vingi tunavyotumia sio salama kimwili na kiroho na usije hata siku moja ukala chakula bila kukiombea, vyakula vingi vinasababisha magonjwa mbalimbali katika mwili , hii inatokana na mambo makubwa mawili moja inatokana na vyakula vingi shetani anakuwa ammesha weka mambo yake, pili sehemu vinakopatikana au vinakolimwa hasa mboga za majani na nyama na vyakula vya kusindikwa hakuna usalama, na ndiyo maana wakati mwingine unaweza ukashanga ukala chakula au kinywaji baada ya muda Fulani unaanza kujisikia vibaya na ukajiuliza inatokana na nini usipate jibu. niliwahi kusikia ushuhuda mmoja kuna mtu alisema kuzimu kuna viwanda vingi kuliko hata vilivyoko duniani na wanatengeneza kila aina ya bidha unayoifahamu mtindo mingi ya nguo,miwani,mafuta ya kupaka n.k, vinatoka huko na vinakuwa na mvuto kwelikweli, mtindo ukitoka kila mtu atatamani awe nao na wanakuwa tayari wamesha nuizia (zindikia dawa)ili kila atakae kula kama ni chakula au atakayevaa kama ni nguo au atakayepaka kama ni mafuta apumbazike akili kwa habari ya Mungu utakuta watu hao wanaouza vitu hivyo wanakuwa na wateja wengi sana na maduka yao yamejaa bidha nyingi na wakati mwingine unaweza usione gari likishusha mzigo, lakini kila siku duka limejaa, sijui kama umewahi kujiuliza vitu vyote vilivyoko madukani unakuta maduka yamejaa kwelikweli hivyo vitu vinaletwa na meli ??!!! sidhani uwezo wa bandari yetu ni mdogo sana meli moja inachukua hadi siku 3 kushusha mzigo na hivi karibuni kulikuwa na malalamiko ya wenye meli kuwa zinakaa muda mrefu kusubilia foleni ya kushusha bidhaa bandarini, hivyo kuna bidha nyingine zinatoka kwenye viwanda vya kuzimu direct na kuja madukani kwa kupitia malango ya kuzimu si kwa meli wala maroli. Kwa upande wa mbogamboga nikisema sana kuna wengine mtaacha kutumia mboga za majani ila kwa ufupi maji yanayotumika si salama, mengi yanatoka vyooni au maji taka ya viwandani ambayo tayari yana sumu (chemicals) maji hayo yanapo mwagiliwa kwenye mboga yanapenya hadi kwenye mboga nazo zinakuwa na sumu hizo ambazo zinasababisha madhala, nyama ndo usiseme hasa kuku, wengi wanafungwa kisasa na wanapewa madawa ili wakuwe kwa haraka na kumbuka hapa mfugaji anachoangalia ni fedha, yuko tayari hata kuzidisha kipimo ili tu kuku au mnyama awe na uzito mwingi ili apate pesa nyingi, na madawa hayo yanabakia kwenye nyama wewe ukila dawa hizo zinaendelea kufanya kazi kwenye mwili wako, utashangaa na wewe unanenepeana kama kuku wa kisasa unapata vitabi visivyotarajiwa na vinaleta madhara kwetu na watoto wetu kama ni mja mzito au kama unavyonyesha, sasa fikiria huyo mtoto wako ambaye yuko tumboni, mfano yeye ataathirika kwa kiasi gani ataathirika mapema mno kuna mtalaam mmoja aliniambia ndiyo maana watoto siku hizi wanavunja ungo au kubarehe mapema kwasababu ya virutubisho vya kukuzia wanavyopewa wanyama vinawadhuru hivi juzi nilisikia kuwa Marekani mtoto wa miaka 9 ameshika ijauzito na kazifungua akiwa na miaka 10 Yaani mtoto ana mtoto na ndiyo maana siku hizi watoto wanaugua magonjwa ambayo zamani watoto walikuwa ni nadra sana kusikia anaumwa. wezi wa February nchini Ujerumani kuna mtu anayefanya kazi kwenye kiwanda cha kutengenezea vyakula vya kuku alikosea akaweka chemicals kwenye chakula cha kuku bila yeye kujua chemical hizo ziliwapata kuku zikaingia hadi kweye mayai waliyotaga nayo yakawa na chemical hizo zenye madhara kwa binadamu, ilibidi mashamba yote ya kuku yaamliwe kuku wauliwe na mayai yaharibiwe. Sasa afadhali wenzetu wana utalaamu wa kugundua madhala yanayoweza kutokea, ni mara ngapi hapa kwetu watu watakuwa wamekula vyakula visivyofaa. Usalama wa chakula unakuja pale tu unapo kiombea na kukitakasa kwa damu ya Yesu, hivyo siku zote mahali popote usile chakula bila kuomba hata kama unalia bar, kuna watu huwa wanaona aibu kuomba mbele za watu kama unatabia hiyo afadhali usile kuliko kula chakula bila kuomba. kuna mtu mmoja alikuwa mchawi akaokoka aliniambia mara nyingi watu wanaokula huwa wanakula na majini pamoja na wachawi na wala wewe huta waona utashanga ulipima kipimo cha kutosha lakini mnakula hamshibi kwa nini kuna mianya, hivyo takasa chakula ili Mungu akibariki mkila mpate afya njema na si maradhi.

Upande wa vinywaji nako hakuko salama asilimia 80 ya viwanda vya vinywaji vinatengeneza viywaji vikali na ni asilimia ndogo ya viwanda vya vinjwaji baridi na mimi nayafahamu makapuni makubwa duniani 2 yanayotengeneza vinywaji baridi ambayo ni Coca cola na Pepsi na vinywaji hivi usiviamii sana maana wote wanao tengeneza ni wamataifa wanaweza kutumiwa na ibilisi kuweka madhara humo mf kinywaji cha cocacola na pepsi zinasadikika kuwa si zuri kwa afya, ijapo watu wengi wanazipenda imetengezezwa na chemicals ambazo zinalea madhara kwa afya na nirahisi sana kupata vidonda vya tumbo kama ukinywa ukiwa na njaa. ukitaka kuamini chukuwa coca cola au Pepsi uimwage kwenye sink chafu la choo baada ya muda hutakuwa na kazi ya kusugua sink hilo maana kemikali zake zimeshayeyusha uchafu wote au chukua Coca au Pepsi ifungue harafu weka msumali wa inch 6 pamoja na mfupa wowote wa mnyama baada ya masaa 76 ukifungua hiyo chupa huttakuta chochote yaani mfuna na msumari unakuwa umeyeyushwa na chemicals zilizoko kwenye soda na mimi kwa macho yangu niliwahi kuona mtu anaosea betri ya gali kwa kutumia coca cola, nilimuuliza akasema inatakatisha na kuondoa uchafu ulio ganda kwenye berti vizuri zaidi kuliko hata maji na sabuni sasa jiulize ni chemicals kiasi gani zimo humo hata kuyeyusha uchafu kwa maana nyingine aheri unywe sabuni ina afadhali kuliko hiyo soda, na si hivyo tu kuna soda za Pepsi za makopo (anglia picha) kuna neno wameliweka kiutaalam sana ambalo kwa akili za kawaida huwezi kutambua (soma kwenda chini utaona neno SEXY) swali la kujiuliza hilo neno lina maana? gani kuna siri gani nyuma ya pazia? na kwanini wameliweka kwenye soda na wasiweke kenye vitu vinavyohusiana na hilo neno nina wasiwasi na haya ni mawazo yangu yamkini kila atakaye kunywa kinywaji hicho apate mawazo ya kufanya tendo hilo na tena si katika njia iliyosahihi ila iliyo kinyume na neno la Mungu. Na ndiyo maana kuna mambo watu wanafanya mpaka kwaakiri tu ya kawaida unajiuliza imeweje huyu kafanya kitendo hichi hupji jibu ni kwa sababu kuna nguvu Fulani imemsukuma(mf kubaka mtoto, kuuwa). Yamkini na wewe utakuwa na mawazo yako mwenyewe “rukhsa” na uone ujanja wao ni mpaka uunganishe makopo mawili ndo lionekane neno hilo, hapo mwenye macho hambiwi tazama ni akili kichwani kwako. kuna mtu aliwahi nimbia kuwa pombe zote zilizoko Duniani zinatengezwa kwanza kuzimu na ile fomula wanapewa wanadamu bila wao kujijua na kuiweka katika vijwaji hapa Duniani na inasababisha watu kupenda ulevi tena wa kupindukia na bila kunywa hajisikia vizuri . Hivyo tunatakiwa kuvitakasa kabla ya kula au kunywa ili kuondoa madhala yaliyo nyuma ya pazia. Hapa sijazungumzia pombe usije ukaiombe ukanya ukadhani kilevi kitaondoka nazungumzia vinywaji na vyakula tunavyoruhusiwa kutumia na kanisa letu. Hivyo ndugu yangu vitu vingi si salama usalama upo kwa Yesu tu hivyo unatakiwa kuwa na upako, maombi wa kuzuia madhara mbalimbai ambayo wanaweza kukupata katika vyakula na vinywaji unavyotumia au la kupunguza kabisa kula vitu hivyo maana utapunguza siku zako za kuishi.ITAENDELEA

Chapisha Maoni