Jumapili, 10 Aprili 2011

JE WAJUA?




Karibu asilimia 80 ya vingozi na watu maarufu wanafanya kazi huku ni wagonjwa wa magonjwa mbalimbali ambayo ni BP, kisukari, ukimwi, kiharusi kansa nk. hii imegundulika baada ya viongozi wengi wa serikali na vyama vya siasa kumiminika kwenda Lolindo kupata kikombe cha Babu Ambikile chenye kusadikika kuwa kinatibu magonjwa mbalimbali na baadae kusema kuwa wamepona. uchunguzi uliofanywa na mwandishi wetu umegundua kuwa wapo viongozi wengine wamekwenda Loliondo kimya kimya bila kuonekana na waandishi wa habari, hii inatia wasiwasi kuwa viongozi hao sidhani kama wanaweza kulitumikia Taifa kwa asilimia 100% kutokana na kusumbuliwa na magonjwa hayo na wakati mwingine serikali imekuwa ikitumia gharama kubwa kwa ajili ya kuwatibia kwenye hospitali zenye gharama kubwa ndani na hata nje ya nchi. Ijapo kila siku zinavyozidi tiba hiyo inazidi kuzua utata hasa baada ya watu wengine kuibuka na kusema nao wameoteshwa mungu dawa hiyo ya kikombe. Maoni ya watu yanatofautiana na yako katika mitazamo miwili wako ambao baada ya mahojiano na mwandishi wetu wamesema kuwa ujio wa tiba hivyo umeweza kuleta neema katika mambo fulani ,alitoa mfano kuwa kwa ccm kwao imekuwa nafuu na wametumia mwanya huo kuwasahaulisha wanainchi kwa habari ya maandamano ya chadema yaliyokuwa yanatishia amani na kuwakosesha usingizi viongozi wa ccm ambayo mpaka sasa hayajulikani yameishia wapi, hii imetokana na vyombo vya habari ambavyo vilikuwa vinatoa support kubwa kutangaza na kuhamasisha maandamano hayo kuelekeza camera na kalamu zao kwenye dawa za kikombe, na kwa ujanja mkubwa ccm wamesuport na kutoa matamko ya kusaidia wanachi kwenda Loliondo ambayo yamefunika kabisa mambo mengine kwenye vyombo vya habari. Na wapo wengine ambao wamesema dawa hiyo ya Babu inauhusiano mkubwa na freemason kutokana na kuwa na mvuto wa ajabu akiongea na mwandishi wetu Mr Rashidi Makongoro mkazi wa gongo la mboto alisema ana wasiwasi sana na dawa hii na inawezekana ikawa na madhara na sijui itakuweje hapo madhara yatakapoanza kutokea maana watu wengi wamesha kunywa pamoja na viongozi wetu akimalizia kwa kunuuku kifungu cha biblia huku yeye ni muslam alisema nabii Issa bin Mariam alisema katika kitabu cha Mat 24:5 unaosema Kwa sababu hiyo wengi waakuja kwa jina langu, wakisema mimi ni kristo, nao watawadanganya wengi. Nanyi mtasikia matetesi ya vita, angalieni msitishwe maana hayo hayana budi kutukia lakini ule mwisho bado. Alimalizia na kusema kuwa yeye anaamini kuwa mwisho wa dunia umekaribia na ndio maana mambo kama haya yanatokea ambayo hayajawahi kutokea hapo nyuma. Kwa upande mwingine hali bado ni tete kwenye kinu cha nyukilia ambacho kinasadikika kuwa ni kikubwa kuliko nyote Duniani baada ya tetemeko lingine kuikumba tena Japan lenye ukubwa wa 7.5 ya vipimo vya matetemeko na kufanya hali ya Japani kuendelea kuwa mbaya na kuhitaji msaada wa kimataifa. mmoja wa wapashaji habari alipasha kuwa katika historia haijawahi tokea Japani kuwa na mgao wa umeme lakini sasa hivi wana mgao. Akiongeana na mwandishi wetu mwalimu mbobevu wa mambo ya kijamii Mwl Prosper Wilbrod alisema kuwa haya ni mapigo ya Mungu kwa nchi hiyo maana wao hawaamini kuwa kuna Mungu na ni mbaya sana kwa nchi kutokutambua uwepo wa Mungu ndiyo maana anaruhusu vitu kama hivyo ili wajue kuwa Mungu yupo. Akielezea habari za mashariki ya kati Mwl Prosper alisema maandamano ambayo yanaendelea yana ashilia vita kuu ya mwisho wa Dunia akifafanua alisema kuwa viongozi watakaoshika madaraka sasa hivi katika nchi za Misri, Tunisia na nchi zingine za kiarabu hawatakuwa na amani na Israeli. na zipo tetesi kuwa nchi za kiarabu zinampango wa kuivamia Israeli kijeshi na kwa upande mwingine na Israeli wakiwa wanajipanga wametengeneza siraha ambayo haipo popote duniani ili kujihami na uvamizi huo, siraha hiyo yenye uwezo wa hali ya juu ya kudaka makombora ya aina yoyote yatakavyo rushwa na adui na kuligeuza na kwenda kuripua lilikotokea inaaminika itasaidi kuwakinga Israeli, kwa upande mwingine Israeli wanaendelea na upanuzi wa nchi yao kila itwapo leo na kuwarudisha waisraeli walioko nchi nyingine ujenzi huo unaofanywa kwa speed ya hali ya juu kwa kutumia muda wa saa 24 kukkamilisha ujenzi wa nyumba, na wanajianda kwa ujenzi wa hekalu ambalo michoro na material yamekwisha adaliwa, na ujenzi huu unategemewa kuchukuwa masaa 24 tu na hekalu kukamilika. Mwandishi wetu alifanya mahojiano yasiyo rasmi na aliyekuwa waziri mkuu na makamu wa kwanza wa raisi wa mwaka 92 Mh Dr John Malecela ambaye ni mbobevu wa mambo ya kisiasa hapa nchini na kimataifa nyumbani kwake sea view alisema kuwa mambo yanayotokea Afrika yanasababishwa na nchi za magharibi ambazo hazina nia njema zaidi ya kutafuta kujinufaisha na kuziacha nchi zilizoingia kwenye machafuko hayo kuwa duni. alitoa mfano wa nchi ya Iraq alisema ni afadhari ilivyokuwa kabla ya Sadam Husseni kuliko ilivyo sasa maana sasa hawana kiongozi thabiti na watu wanakufa ovyo kila siku tena wengi kuliko hata hao aliouwa Sadam wakati wa utawala wake. Akiongelea kwa habari ya Libya alisema kuwa hata Gadafi hawezi kuhimili shinikizo la nchi za magharibi ni bora asamli amri tu. ila akongeza kusema kuwa Libya nayo haitapata tena kiongozi kama Gadafi. Alipoulizwa kwa habari ya Tanzania, kama nchi za magharibi zinafanya kwa Afrika Tanzania itapona? alisema usalama ni mdogo na usije kushanga kuwa hayo yakaja kutokea hata hapa Tanzania nchi za magaribi zinaweza kusema kuwa tumechosha na utawala wa CCM tunataka tuone mabadiliko wakatafuta chama cha upinzani wakaanzisha vulugu alimaliza.


Haya wewe uliyesoma mambo hayo utakuwa umepata kitu hebu tuombe kwa amani ya Dunia, Afrika na Tanzania Mungu atunusulu na mambo haya yanayoendelea na Mungu atupe macho ya rohoni tuelewe nyanayoendelea yanamaanisha nini katika ulimwengu wa roho Amina.


















Hakuna maoni: