Jumapili, 10 Aprili 2011

Maoni ya wasomaji

kama kawaida mawazo yenu mnayotuma huwa napenda kuyaweka wazi ili kupanuana mawazo yote katika kuujenga ufalme wa mungu Mungu awabariki naotuma maoni yenu.

Ubarikiwe sana, kwa ujumbe wenye kugusa maisha yetu kwa ujumla, yote yaliyomo kwenye ujumbe, ndiyo ukweli wa maisha yetu.
lakini mimi naona kwa mtazamo wangu kuna baadhi ya watu hawaabudu kazi, maana hata wasio na kazi za kuajiriwa pia nao wako busy, kuhangaika na kuchoka sana. Kwanini hali ya maisha imekuwa ngumu sana, imani ya kuamini neno la Mungu pia imepungua , watu wengi wanatembea kwa kuangalia ishara, apate kwanza fedha ya kula, ikibaki ndiyo aangalie kama inatosha nauli na sadaka ya kwenda kanisani, vile vile hali ya DSM ni kero kwa upande wa foleni, hasa kwa wale wanaokaa nje ya mji, muda mwingi unatumika kwa kutembea , hata kama mtu alitamani kwenda kanisani muda utaisha akiwa kwenye foleni. jambo jingine ambalo limechukua sehemu kubwa ni haya matangazo yanayotolewa na radio za dini kwa habari ya semina, mikutano mkubwa na maombi watu wengi wanakuwa huko. Na sadaka wanatoa , michango ya kupeleka injili na wana mtegemeza mtumishi na ufalme wa Mungu unajengwa. hiyo ni changamoto sana kwa watumishi wa Mungu. hasa kwa kipindi hiki cha utandawazi, ambacho kwenye internet kuna kila kitu, naweza nikasikiliza mafundisho, maombi na maombezi mpaka mwisho , nikiwa ofisini na nikahisi uwepo wa Mungu, lakini imetupasa tukutanike pamoja na kwa umoja huku tukisimama katika neno la Mungu.


Mungu atusaidie ujumbe huo ulete mabadiliko katika maisha yetu.

Irene kipwate.
Chapisha Maoni