Jumapili, 3 Aprili 2011

KWA MTINI JIFUNZENI


Kuna siku moja wanafunzi wa Yesu walimuuliza kwa faragha wakisema tuambie, mambo hayo yatakuwa lini? nayo ni nini dalili ya wakati, hayo yote yatakapokuwa karibu kutimia? Mat 24:3 – 51, Mark 13:3 – 37. Maadiko haya yanazungumzia kwa habari ya mwisho wa dunia ukisoma kwa roho uagundua tuko mwisho wa mwisho wa dunia mimi nijuavyo kanisa la kwanza waliishi siku za mwanzo wa mwisho wa Dunia sijui kama umenielewa kinachonishangaza ni kuwa wao waliamini kuwa kabla wao wawajafa Yesu atakuwa amerudi na ndiyo maana hawakupoteza muda wao hovyo hovyo kila wakati walihimizana kwa habari wokovu na kurudi kwa Yesu, wakikusanyika wanakumbushana na kuagana na salam ya MARANATHA yani Bwana wetu anakuja. Hofu hivyo ilikuwa nzuri iliwafanya kila wakati wajitakase na kuwa watakatifu bila waa na ilitokana na maneno makali yaliyoko kwenye vifungu hivyo hapo juu na mi nakumbuka wakati nikiwa mdogo makanisa yalikuwa na hofu hiyo na kulikuwa na mafundisho mazuri ya kuukulia wokovu na kuishi maisha matakatifu na mikesha yenye upako inayoleta taswira kuwa Yesu anaweza kurudi wakati wowote watu walikuwa na hofu ya Mungu mtu kutengwa kanisani kwa kufanya dhambi mambo haya yalikuwa adimu sana zamani hizo mtu akitengwa watu wanalia wanamwombea rehema ili mtu huyo arudi kudini si kama siku za leo watu wengi wanatengwa na ndo kwanza watu wanafurahi na kucheka.
            Ukisoma tu maadiko haya kwa akili ya kawaida hutaacha kuunganisha na matukio mengi yanayotokea sasa, Yesu alisema watakuja wengi kwa jina langu hayo tumesha yaona wametokea akina yesu wengi tu na kuna mmoja hata aliwahi kuja kanisani kwetu Magomeni na alipopewa nafasi ya kujitambulisha akasema yeye ni yesu. Kwa habari ya vita ndo usisema kila kukicha vita vilianza Kuweiti ,sudani, Liberia, Somalia,Iraq na vita vinavyoendelea sehemu mbalimbali Duniani kama Libya n.k mwenye kuelewa maandiko hautashanga maana hayo yahana budi kutokea, kutakuwa na njaa kila mahali wewe ni shahidi nafikiri umesha wahi kuona watoto wa Somalia ambavyo wamekonda kwa kukosa chakula na si Somalia tu hata hapa kwetu Tanzania inatokea mara kwa mara tu kunakuwa na njaa, matetemeko ya aridhi yanachanganyika na Katrina tsunami kama yaliyotokea Japani mpaka unaweza kudhani ni mambo ya kuacti jinsi nchi yao ilivyoharibiwa na tetemeko lilichanganyana na Tsunami mpaka sasa hali ni tete mitambo ya nyukilia imewashinda kudhibiti ni hatari sana, kumekuwa na manabii wengi wa uongo maasi yameongezeka ubakaji,mauaji ya alibino, uchunaji ngozi watu,ujambazi watu wanajiua hovyo, maandamano yanayofanyika katika nchi za uarabuni na sekeseke la wanganga walioibuka kwa staili ya (cup of life) kikombe sasa hivi yuko Babu wa Loliondo, dada wa Taboa, Kaka wa Iringa na kuna mwingine yupo Moshi wote hawa wanajaza misululu ya watu kuwa wanaponya magonjwa sugu kwa staili inayofanana na kudai kuwa wameoteshwa na Mungu.

            Ukija upande wa pili wa tekinologia nako kuko vizuri kurahisisha mawasiliano pindi mpinga kristo atakapoanza kazi mapinduzi na maandamano yanayofanyika sasa hivi watu wanapashana habari kwa kupitia mtandao tu we unashanga watu wako mtaani wanaandama sasa hivi mtu anaweza kutua ujumbe kwenye mtandao ukaenea dunia nzima kwa muda mfupi kwa wale mnaotumi facebook ulitokea uvumi kuwa facebook itafungwa kwa muda furani ujumbe huu ulisamba dunia nzima kwa muda mfupi tu, vitu ya mawasiliano vianashuka bei kila leo sasa hivi watu tunaongea kwa robo shiringi ya Tanzania ajabu!!! Na tunasema kuwa hela ya Tanzania haina thamani computer zinapatikana kwa wingi sana mtandao nao bei rahisi na kuna waya ambao utapita Dunia nzima na umeshafika Tanzania fiber cable ambayo itarahisisha zaidi kupunguza bei za kutumia mtandao na kila mmoja anajitahidi ajue ili asionekane amepitwa na wakati (mshamba)kumbe tunaanda mazingia na haikwepeki!!!. Television na vituo vya redio kila sehemu na vingine vinakosa hata habari za kutangaza wanakuwa wanaongea mambo yanayopotosha jamii tu. Barabara nazo zinajengwa kila kona tena na wafadhili ili kuiunganisha Afrika kwa barabara hii nayo ni maandalizi, na kuna tetesi kuwa mji unaojengwa Kigamboni ndiyo yatakuwa makao makuu ya east Afrika ya mpinga kristro utakua ni mji wa kisasa wenye kila aina ya vivutio.
            Tuje upande wa pili je kanisa liko macho kama ilivyokuwa kanisa la kwanza? Kwa upande wangu naona kuna mapungufu mengi mafundisho yenye nguvu za Roho mtakatifu yamekuwa adimu wahubiri wengi sasa hivi wanahubiri mafanikio badala mafundisho ya kukulia wokovu, nguvu za Roho mtakatifu, wala habari za kurudi kwa Yesu hutasikia zikifundishwa, na  kuwa maisha ya wokovu ni ya kujikana kuna kukataliwa kutengwa kuteseka hutasikia, habari za mwisho wa dunia, jehanamu ya moto kuwa watenda maovu watatupwa motoni na watenda mema kuvikwa taji, na kwamba  kuna nini baada ya maisha haya ya sasa.namkumbuka Askofu Kulola mahubiri yake ukiyasikiliza utafikiri Yesu anarudi kesho na akielezea jehanamu ilivyo sidhani kama utaleta mchezo kwenye wokovu utaenda jehanamu. wachungaji wa zamani walikuwa wanafundisha maisha baada ya kufa walifundisha kuishi maisha ya kijikana ili baadae tuishi maisha mazuri lakini wachungaji wengi wa sasa wanafundisha maisha mazuri hapa Duniani kufanikiwa kifedha kupanda ndege, kwenda Ulaya utafikiri ulaya ndiko mbinguni. na kutokufundisha kabisha kwa habari ya maisha baada ya kufa. kwa mtindo huu wengi wameokoka kwa kufuata mafanikio kwa Yesu na si vinginevyo na kwa sababu hawana msingi wa neno la Mungu ndiyo wanaoharibu kanisa wakikutana na magumu wanarudi nyuma wengine wanaanguka dhambini. kutangatanga makanisani kutafuta mafanikio. sijui labda kwa sababu Yesu Mat 24:12 na kwa sababu ya kuongezeka maasi, upendo wa wengi utapoa. Upendo haupo tena kanisani tunabaki tunatamkiana kuwa tunapendana lakini hatuonyeshi kwa vitendo na kuna matabaka kanisani na gepu ni kubwa la wenye uwezo na wasio na uwezo na kama ingetokea Mungu aseme tufanye kama kanisa la kwanza kuwa tufanye vitu vyote kuwa shirika tuumege mkate kwa pamoja sidhani kama wapo watakao kubali. Binafsi wakati mwingine inanipa maswali mengi wakati mwingine kuwa kwanini sasa hivi naona kanisa ni dhaifu? Hili ndilo kanisa Yesu alilosema atalijenga katika mwamba ulio imara wala nguvu za kuzimu hazitalishinda  au je? amri mpya Bwana aliyotuachia ya upendo ndo hii au je kuwa kanisa la kristo ni mwili mmoja na sisi ni viungo ndani yamwili ya kristo kama ndo hivyo kazi ipo maana kila kiungo kina jitenga na chenzake kinajiona chenyewe ni bora kuliko kingine ushirika haupo kabisa badala ya kanisa kuongezeka nguvu ndo kwanza ni kama limeduma niliona takwimu za uislam wanaongezeka kwa kasi sana kupita wakristo kuna vitu vingi sasa hivi vinakuwa adimu katika kanisa kama unabii, uponyaji, siku hizi hata mikutano ya injiri semina inadorora sio kama zamani mahudhurio ni hafifu siku hizi hata makusanyiko ya kanisa la TAG si kama zamani kila kanisa la mahali pamoja wana mambo yao wenyewe, idara nazo zina hali mbaya, kuwaleta watu kwa Yesu siku hizi imebakini simulizi kwa ujumla kanisa lina hali mbaya sijui wewe unatazama kwa mtazamo gani mimi na amini kuwa kama Yesu angezaliwa kipindi hiki ambako tekinologia imekuwa hivi angefanya mambo mkuu zaidi na angekusanya watu nafikiri Dunia nzima ingeokoka na kusingekuwa na mambo yanayotokea leo watu kukimbia kanisa na kukimbilia kwa Babu au Dada kupata uponyaji maana waupata kanisani.
            Basi kwa mtini jifunzeni unapoona unaanza kuchanua ujue wakati wa mavuno umekaribia kwa changamoto hii ikufanye usonge mbele na kuongeza bidii katika kristo tukeshe maana hatujui ni siku ipi na saa ipi atakayokuja mwana wa adamu. Kama ni dalili karibia nyingi zimeshatimia  Maranatha.

Maoni 1 :

Unknown alisema ...

SHALOM MARANATHA.
Kwakweli hili inabidi liwafikie wakristo wote tunaosema tumeokoka,tunamjua Yesu na tuko tayari kunyakuliwa pamoja naye ile siku ikifika.nilikuwa natafakari na mimi hsyo yote ni kweli siku hizi mikutano ya injili kwa ajili ya kuwahubiri watu habari njema haipo.tumebaki nakanisani tunatiana moyo hata kwenye vitu ambavyo ni mtu personal unatakiwa kushuhulika na maisha yako kama ni uponyaji au ni dhiki angalia neno linasema nini juu ya hayo yote.
Ila hatukumbushani juu ya habari ya kurudi kwake Yesu,ukisoma pia mat 24:32-34 inatuonyesha kuwa tukiyaona hayo yote tujue kabisa yuko milangoni,na inasema kizazi hiki hakitapita hata hayo yote yatakapotimia,maana yake ni nni?hki kizazi tulichoko hakitapita watakatifu tutakuwa pamoja nae siku moja na kizazi hiki hakitapita ile miaka 7 ya dhiki kuu pia kutimia kwa wale ambao hawakumwamini kwa neema hii ya sasa.
.nimekuwa nikiendelea kujiuliza maswali na kujijibu mwenyewe,yakwamba wakati yesu aliposhuka kwa wanadamu kwa ajili ya ukombozi na mpaka akajidhihirisha kwa wanafunzi wake wapo ambao bado hawakumsadiki,pia sikuishia hapo nikawa nasomo kitabu cha kutoka jinsi mungu alivyokuwa akitembea na wana wa Israel neno lilkuwa linasema mara nyingi Mungu aliufanya moyo wa farao kuwa mgumu kuwaruhusu wana wa Israel kutoka kwenda kumtolea Mungu sadaka na kumfanyia ibada,bado haikuishia hapo kwenye agano jipya Yesu akawa anaongea na wanafunzi wake anasema kati yenu yupo atakaenisaliti kabla jogoo kuwika hii ina maana kumbe Yesu alijua kila kitu sasa swali ni kwamba kwanin asingemzuia au angemtoa amwambie ni wewe kijana naomba ujitenge nasi au amtaje pale ila nikajijbu na kusema kumbe aliyaacha haya yote yapate kutimia maana ndivyo neno linavyosema kwahiyo Mungu kuna mambo ameyaacha yatokee kwasababu hayana budi kutokea maana ndo neno linaksmilishwa.

Hivyo basi ndugu zangu tuonapo haya turejee tutafute nguvu za Mungu maana ndizo pekee zinaweza kutuponya(kutukomboa)na haya yote.neno linasem Mungu kwetu sisi ni kimbilio na nguvu msaada utakaoonekana wakati wa mateso,magumu,dhiki n.k.
Na pia neno linasema duniani mnayo dhiki lakini jipeni moyo maana mmeushinda ulimwengu.maana yake ni kwamba Mungu anajua anaelewa na anaona ugumu uliopo kwa wanadamu lakini anazungumza na kusema tumeushinda ulimwengu maana yake hakuna kitu cha kutushinda.


Wakati mwingine nitaomba tusaidiane na kufundishana juu ya ibada ya kweli.kuabudu,kusifu(worshiping)hapo kuna tatizo sana kwenye kanisa la sasa.nawapenda.