Jumatano, 30 Machi 2011

Maoni ya wasomaji

Mungu awabariki kwa wale mlioweza kuchangia mada hii najua inatusaidia kupanuana mawazo na haya hapa chini ni baadhi ya maoni wasomaji kama ifuatavyo.

Mpendwa,
Suala la kwamba wimbi hili litatufikisha wapi hilo si la msingi, cha msingi ni kuangalia wapi ambapo kanisa halikusimama katika nafasi yake. Umati unaofurika Loliondo ungeweza kufurika katika makanisa ya kiroho endapo kanisa lingetoa suluhisho la matatizo yao. Watu ni wagonjwa lakini wanahubiriwa, wanaombewa, wanafunga, wanafanya maombi ya jumla na yao binafsi lakini hawapati suluhisho la matatizo yao. Tunahubiri Yesu anaponya lakini watu wanaingia makanisani na magonjwa yao na wanatoka nayo kurudi nyumbani. Njoni Kwangu ninyi wenye kulemewa na mizigo, Math. 11:28, lakini watu hawaoni mizigo yao kutuliwa.

Sasa Babu wa Semunge endapo anawaponya UKIMWI na magonjwa mengine yaliyoshindikana mahospitalini na kwenye maombezi watu wafanye nini wakati wanahitaji kuponywa?

KANISA LIJIANGALIE WAPI HALIJACHUKUA NAFASI YAKE. TUMTAFUTE MUNGU TUACHE SIASA MAKANISANI.

Mzee Lumelezi
 
changamoto ni kwamba watu wamekosa matumaini, na kwa idadi hii inaonyesha kweli duniani watu wagonjwa, kanisa lina kazi ya kuwarudishia watu matumaini ya Yesu ndiye bwana na ni mponyaji, na hakika kwa idadi hii wa wagonjwa litokee azimio kwamba hakuna kulala hadi kieleweke. Ukweli kizazi  hiki kinahitaji ishara na maajabu na wala si mafndisho, na hakika watu wataangamia kwa kukosa mafundisho,Mungu ambariki Mwakasege na watumishi wengineo watoao mafundisho kwa watu, Amina.
 
Charles Mwaihojo
 
Kwa suala hili la tiba ya babu limebaki kwa mtu binafsi moyoni mwake anajisikiaje, juu ya hiyo dawa
maana hata likitolewa tamko na viongozi wetu wa TAG kwa mtazamo wangu kulingana na watu wanavyo kwenda kwa babu na kurudi na wengine ni wapendwa,
sijui kama hilo tamko wote watalielewa. mfano mtu ambaye ameteseka kwa ugonjwa wa sukari kwa miaka mingi na amesikia kuna dawa toka kwa Mungu utamwambia maneno gani mpaka akuelewe?
na kibaya zaidi watu wengi wamejengewa imani kuwa ile dawa haiponyi ila neno la Mungu linalosemwa na mchungaji mstaafu kabla ya kukupa hiyo dawa, ndilo linalo ponya. ukichota mwenyewe ile dawa ni sumu kali sana. !! hiyo ni changamoto kwetu !!
NI wapi tulipotoka, wapi tulipo na wapi tunapokwenda. Mungu atusaidie tumwangalie yeye kupitia neno lake.

Ubarikiwe Irene Kipwate

hayo ni mawazo yaliyotolewa lakini Mch Kanemba nae hakunyamaza kimya juu ya ya kikombe cha babu(cup of life) ametoa ufafanuzi katika ibada ya j2 kuwa watu walitegemee neno la Mungu na si vinginevyo akiongea kwa msisitizo live kutoka South Africa amewataka washirika kutokuyumbisha na imani nyingine.

kwenye mtandao nako vituko vingi vinavyohusu babu na kwa sasa kuna watu wasiopungua 6 waliokwisha jitangaza kuwa nao wanatoa tiba kama za babu kwa mtini Yesu alisema tujifunze!!!! ubarikiwe.
Chapisha Maoni