Jumatano, 16 Machi 2011

DAWA YA BABU INAYOPONYA MAGONJWA SUGU WAPENDWA TUTAPONA?

WAPENDWA TUTAPONA NA WIMBI HILI?


Katika siku za za hivi karibuni kumekuwa na habari zinazomuhusu mganga maarufu mwenye dawa inayoponya magonjwa sugu kama ukimwi, kisukari,kansa, BP n.k mchungaji mstaafu wa KKKT Ambilile Mwasapile ali maarufu Babu. habari zake zimeshika hatamu kwenye nyombo vyoote vya habari hapa nchini na nje ya nchi hakuna chombo hata kimoja ambacho kitaacha kuweka habari hizi na zisipo wekwa halitauzwa kwa kufanya hivyo imesababisha Babu kuwa maaruku kila kukicha kwa kila mtu na ndo maana hata viongozi wa nchi nao wameenda kunywa dawa na kutoa ushuhuda unaosababisha watu wengi kwenda, hivi kweli kama mbunge wako au kiongozi wako uliyemchagua kasema kapona wewe utasubiri nini kwenda na viongozi haohao wengine wamediriki hata kutoa usafiri bule kusaidia watu zaidi ya hapo na serikali yetu nayo imebariki kwa kutoa ulinzi na usimamizi wa kutosha kuhakikisha watu wanahudumiwa na zipo taarifa kuwa hata wageni kutoka nje ya nchi wanakuja kutbiwa kwa Babu. Umaarufu bwana unakuja kwanjia nyingi sana nani alimjua Babu mwaka 2009 hakuna, sasa ni maarufu na hata ikitokea akafa leo atazikwa kwa hesima kubwa na watu maarufu.JE DAWA HIYO INAPONYA KWELI?.

Siku zote anayepigwa na jiwe ndiye anaye lalamika au aliyenyeshewa na mvua ndiye msimuliaji mzuri kuna uwwezekano ikawa inaponya lakini kwa imani yetu bado haitafaa kutumika kutokana na mazingira yake hatukatai kweli kuwa kaoteshwa na Mungu ila ijulikane kuwa kuna miungu wengi hivyo kutaja mungu sio kigezo cha kuamini kuwa ni Mungu tunayemwabudu. Labda nikupe kisa kimoja ambacho mimi mwenyewe nilikishuhudia miaka 2000 kulikuwa na mama mmoja ambaye tulimshuhudia na alikubali kuokoka ila ikawa ngumu kwake kuhama dhehebu lake mda si mrefu aakawa anasikia sauti inasema nae na kudai kuwa ni sauti ya mungu baada ya sisikupaa taarifa hiyo ilitushangaza sana na ikatokea siku moja akaja nyumbani na kutushudia hayo kuwa mungu anasema nae baada ya mazungumuzo tuliamua kufanya maombi cha ajabu Yule mama alilipuka pepo za ajabu na wakati tunakemea ndipo pepo zilisema zilitumia mbinu hiyo kwasababu ziliona zitampoteza mtu wao hivyo tulizikemea na kutoka na mama akafunguliwa. Hivyo basi inatakiwa kuipima kila jambo ambalo linakuja kwenu na neno la Mungu ilikupata ukweli hata kama inaponya dawa yake sitaitofautisha na waganga wengine wa jadi kutokana na maingira inavyopatikana na kutayarishwa.PICHA YA MCH MSTAAFU WA KKKT MWASAPILE(BABU) MGANGA MWENYE DAWA INAYOTIBU MAGONJWA SUGU.

JE? TAG TUTAPONA.
Baada ya utangulizi huo nirudi upande wa pili wa shilingi kwa habari ya kanisa hasa walokole hii ina changamoto gani? kwa mtazao wangu finyu nilipanua ubongo wangu kwanza kuwaza kwa habari ya wapendwa, makanisani tunao watu wengi wenye magonjwa ambayo tunaambiwa kwa dawa ya Babu ya kikombe kimoja cha chai cha sh 500 ambayo ni gharama ya kuandikisha mgomjwa katika hospitali za serikali mtu anapona kabisa!! Wapendwa hao labda walishaombewa na kuombeaga, kufunga na kufungaga lakini bado ni wagojwa wa magonjwa yao mpaka wengine wanatumia maandiko kusema kuwa huu ni mwiba wangu wamekata tamaa ya kupona kabisa magonjwa yao na huku wanaambiwa kwa Babu 500 tu unapona ugonjwa wake ambao umemtesa kwa muda mrefu hivi mtu kama huyu akikuomba ushauri kuwa aende kwa Babu akapate nga kikombe hicho kimoja apone utamshaurije? Wewe wajuwa na mimi najua ambavyo nitamshauri na ninajua kuwa hapa majibu ni mawili wenginie watasema aende na wengine mtasema asiende!! Nafikiri wakati kama huu inatakiwa viongozi wetu wa kanisa watoe tamko kama ambanyo wa KKKT kwa kupitia Askofu Laizer waliwaita waandishi wa habari na kuwaambia kuwa wao wameibariki dawa hiyo na ni ruksa kwao kuitumia na ninaamini ijapo yeye sie Askofu mkuu wa KKKT nahisi alimshirikisha mkuu wake ili kutoa tamko hilo na Mch kakobe nae katoa msimamo wake. nikurudi kwetu huku TAG tunahitaji tamko kabla wimbi hili lenye kasi kama za tsunami halijawakumba wengi na tusishangae kusikia kuwa wako ambao wameshakwenda kwa babu kimya kimya kupa matibabu. Nakumbuka miaka kama 3 au 4 iliyopita kanisa letu lilitoa msimamo kuhusu vinywaji visinyo na kileo vinavyotengenezwa na mampuni ya bia kuwa ni marufuku kutumiwa na wa TAG, ni kweli ilituponya wengi ijapokuwa kuna ambao walisha anza kutumia na wameshindwa kuacha mpaka leo Bado kwetu tupate msimamo wa vingozi wetu, usinishangae na usiniulize kuwa sina roho mt ninae ila tunapokuwa na viongozi lazima tusikie sauti zao katika mambo yenye utata kama hili kama wapendwa wa leo kila kukicha wana badili makanisa kutafuta miujiza ije hili ambalo nyombo yote vya habari vinalitangaza bule bila Babu kulipa hata sent 5, nilifuatilia mada ya katibu mkuu alifafanua vizuri kujua kweli ni dawa ya muujiza kutoka kwa Mungu au la ila hakutoa tamko kama la kwenye vinywaji ili tusikumbwe na wimbi hili la Loliondo.
Chapisha Maoni