Jumamosi, 26 Februari 2011

Mganga wa Kikwete Aokoka

Jana nilikutana face 2 face na mganga wa kikwete ambae amekuwa akimsaidia
kushinda nyadhifa mbalimbali Kwa jina anaitwa Yasini Ally kwa sasa anaitwa
Paulo. Katika mazungumzo ya kama dk 20 hivi alieleza kuwa baada ya
kumwezesha JK kupata uwaziri alijengewa nyumba ya kuishi hapa Dar na
aliposhinda uraisi alijengewa nyumba nyingine huko kijijini kwao.
Nilipomuliza walifahamianaje alieleza kuwa yeye na JK ni mtoto wa mama yake
mdogo na yeye alilithishwa uganga (mikoba) na babu yake akiwa na umri wa
miaka 8 hivyo aliacha shule akiwa na darasa la kwanza ili afanye kazi hiyo
ya uganga.

IMEKUWEJE HADI KUOKOKA?
Kuna ndugu yao alifariki ghafla huko Tanga na ilionekana kuwa aliuliwa
kichawi hivyo yeye akapewa jukumu la kulipa kisasi na kwa ustadi wake yeye
alisema angeuwa watu 5 na aliyehusika angekuwa wa 6 hivyo vitu kwaajili ya
kazi hiyo vililetwa ambavyo ni mbuzi 1 na njiwa usiku wakati amelala
akaoteshwa ndoto ya ajabu kuwa alichukuliwa na kuonyeshwa jehanamu moto
mkali unatisha na akaambiwa watenda maovu wote na shetani na baadae
akaonyeshwa mji mzuri sana unapendeza na akaambiwa kuwa mji huu ndio watakaa
wale watenda mema. Asubuhi yake kulivyokucha watu walikuja ili wafanye ile
kazi yao ila akawaambia sitafanya kitu chochote walivyomuuliza sababu
akawajibu hata nikiwasimulia hamtanielewa ila mjue sitafanya na uganga
naacha sitaki kufanya kazi hizi tena. Walimshangaa sana na mara moja na
kujulishwa na alipoongea nae kwenye simu alionyesha msimamo wake huo
ikaamriwa asiingie ndani na avuliwe hadi nguo alizo vaa na afukuzwe alitii
na akawaambia wachukuwe tunguli wote wakaogopa ikabidi azibebe na kuondoka
nazo akiwa na bukta tu na tunguli zake.

SAFARI YA KUTAFUTA KANISA
 Alitembea kwa mguu umbali mrefu kwasababu hakuwa na nauli na safari yake
alikuwa anaelekea Dar kwenye makanisa ya watu wa Mungu alivyofika Chalinze
aliwaomba trafiki wamsaidie apate usafiri wa kwenda Dar walimpiga mkwara na
walipokagua mzigo wake na kukuta ni tunguli waliogopa sana na kumtafutia
rifti ya kuja Dar alipofika alifikia kanisa (nalihifadhi) akasikia sauti
ikimwambia sio hapo ondoka, akaondoka na kufika Magomeni mapipa na kwa
bahati nzuri akona kanisa la TAG Magomeni na akaingia na kueleza yote na
kuanza kupewa huma ikiwa na kuchoma mzigo wake wa tunguli zake na kwasababu
amefukuza akapewa hifadhi.

 baada ya siku kama 2 alikutana na mtu aliye wahi kumtibia zamani
wakasalimiana na Yule jamaa akamwambie we mganga wangu unatakiwa uokoke
uanchane na uganga akamjibu mbona nimesha okoka nimeachana na uganga basi
akamkalibisha nyumbani kwake Tegeta. Kesho yake alikwenda na kuonana na huyo
mwenyeji wake baada ya mazungumzo akampigia simu mch wake kumjulisha kuwa
mganga wake ameokoka mch alikata simu na baadae akapiga na kumwambia kuwa
kuwa Mungu amemwambia amsaidie huyo mganga na akamtaka saa hiyo hiyo
ampeleke ofsini kwake hata kama hana nauli, waliondoka na kufika kwa mch na
waliongea mambo mengi na walienda nyumbani kwa huyo mch kula chakula cha mch
(na huyu si mwingine ni Mtume Mwingila)baada ya hapo akamwambia yeye
atamsomesha uchungaji hivyo wakutane kesho yake.

Kesho yake alikutana na Mtume na kumpeleka kweny chuo chake cha kibaha na
kutembeza na kumkabidhi kwa wallimu. Na hivi leo ndo ameondoka kwenda chuoni
kwa masomo. Kwa kifupi ana shuhuda nyingi ambazo mda hautoshi kueleza
ashukuliwe Mungu anayeweza kufanya mambo makubwa kuliko hile tuombavyo na
tuwazavyo. Ameni (sijafanikiwa kupata picha zake nikizipata nitazileta).

Tuendele kuomba maombi yetu si bure Mungu yuko kazini nasi tusilale tujitie nguvu katika kristo.
.

Chapisha Maoni