Jumatano, 18 Agosti 2010

TUNAWAPA WATOTO WETU MAFUNDISHO BORA?

halom wapendwa,
Ni kweli yatupasa kufanya hivyo kwa watoto wote na si wale tuliowazaa tu. Tukianzia nyumbani.
SHIDA KUBWA ILIYOPO SASA.

- Wazazi tunakosa muda wa kukaa na watoto. Tunatoka alfajiri na kurudi usiku.
Week end vikao na mishemishe kibao za mjini. Mapenzi kwa watoto yapo lakini tumekosa ukaribu na muda wa kukaa nao hata kama tunayo ya kuwafundisha/ kuwaelekeza na kuwafafanulia. Tunajua majukumu sawa je tunayapa muda mzuri?
- Hakuna maandalizi ya kuwajenga watoto katika makuzi yao yanayostahili. Mtoto toka anapoanza kujitambua na kutambua wengine anapaswa kujengwa na kuandaliwa tangu mapema. Hili si jambo dogo na linalopendeza kama lisipopata nafasi mapema. ( Ndio kuna kale kausemi samaki mkunje angali mbichi)
- Kwa kukosa muda watoto wanapata malezi na kujifunza mengi toka kwa watoto wenzao (majirani na mashuleni) pia wanajifunza mengi kutoka kwa wasichana wa kazi. Hadi mzazi ugundue kuwa mtoto anatambia ambayo si nzuri ni baadae sana na huenda ni wakati uko mapumziko ya likizo au la.
HATUJACHELEWA. KWA MUNGU YOTE YANAWEZEKANA. TUANZIE WAPI SASA? TUANZE NA LIPI? NA KWA NJIA ZIPI? NI LAZIMA TUFANYE KITU.
- TUMUOMBE MUNGU JUU YA SWALA ZIMA LA MPANGO MZIMA KABLA YA KUANZA LOLOTE.
- Tupate muda wa kutosha kuwasoma na kujenga urafiki zaidi ya ilivyo sasa. Hii itatusaidia kujua tuanzie wapi. Tusipojipanga vizuri kwenye hili mwanzo wetu utakuwa mbaya na matokeo yatakuwa mabaya.
- Nafasi nzuri zaidi ni ya kuweka ratiba kwa kutenga muda mzuri bila kuingiliwa na jambo lingine labda kwenda sehemu tulivyo. Baada ya michezo na chakula kizuri. Maongezi yanaweza kuanza kwa kusoma mazingira ya watoto au mtoto.
Ni jambo jema kujiandaa kama mzazi na pia kumuandaa mtoto. Hii itasaidia kupokea lolote mtoto atakalotamka hata kama litakuuzi sana utaweza ku control hasira na urafiki kuendelea ili tu utimize lengo la mazungumzo.
Tutambue kuwa unaweza ukawa unaongea kitu au jambo sahihi,
kwa mtu sahihi lakini ikawa si mahali sahihi = 0.

Haya ni muhimu sana kuzingatia.

Natoa hoja

                                                          Familia Nzuri ya Blandina


Na wewe je una mtazamo gani kuhusu malezi ya watoto?

Hakuna maoni: