Ijumaa, 20 Agosti 2010

TUNAWAPA WATOTO WETU MAFUNDISHO BORA?

Jamani unajua Martin tatizo hapa ni kwamba sisi wazazi tunaubinafsi sana na kujisahau. Kwanini nasema hivyo
i. Tunajitafutiaga masemina sisi wenyewe tu
ii. Tunajisahau kwamba tunatakiwa kuwafundisha watoto wetu Kristo
iii. The way tunavyoishi mtoto anakosa cha kujifunza zaidi ya kuiga tabia zetu ambazo hazimfundishi tabia nzuri kwa sababu mtoto anaelewa haraka sana kwa kuiga kile anachokiona na akili zake zinamtuma kila anachofanya mzazi ni sahihi.
iv. Tunaacha kufundisha watoto wetu wenyewe wakati wakiwa katika umri mdogoambapo ni rahisi kushika na kutosahau kama neno la Mungu lisemavyo tunapeleka boding schools wakiwa na umri mdogo wakafundishwe na tamaduni tofauti tofauti kwa sababu zaidi ya masomo pia kule kuna watoto ambao kwao wanaiga vitu vya ajabu na kuleta shule na mwanao anaona/kusikia na anaiga nayeye.

Tumaini

Hakuna maoni: