Ijumaa, 13 Agosti 2010

TUNAWAPA WATOTO WETU MAFUNDISHO BORA?

Tanzania bado ina mambo mengi ambayo bado hayajakaa sawa na wala bado hayatazamwi kwa upana au mtazamo endelevu ukilinganisha na mataifa mengine yaliyoendelea na yanayoendelea, na wakati mwingine tunatilia mkazo mambo ambayo kwa mtazamo wa mbali hayatusaidii lolote. Jambo ambalo ni la mhimu na hayatiliwi ni elimu ya malezi ya watoto. Tunaposema kuwa watoto ni taifa la kesho inatakiwa tumaanishe kweli kweli na tuweke msingi wa hilo taifa la kesho. Nitoe mfano wa inchi ya China watu hawa wajua nini maana ya Taifa la kesho na ndio maana watumia gharama kubwa kuwafundisha watoto kwa habari ya uzalendo, uchapa kazi na ukakamavu na ndio maana wanafanya kazi kama mchwa na inawaletea maendeleo makubwa katika nchi yao. Lakini hapa kwetu sivyo ilivyo jukumu la malezi ya watoto wapo kwa wazazi tu na kwa mtazamo wangu ninamini kuwa sio wazazi wote wana uwezo wa kuwafundisha watoto maadili mazuri na je watoto yatima watafundishwa na nani? Nafikiri kuna haja ya elimu kufundishwa kwa watu wote hasa wazazi namna ya kulea watoto au hata walimu wa shule za awali msingi na hata sekondari. Haya nimeyapata baada ya kuhudhuuria semina nzuri ya pekee yenye mafundisho adimu iliyoendeshwa na Mwl Wilbrody Prosper.akifundisha kwa umakini na kwa kipaji alichopewa na Mungu alifafanua kwa upendo ili kila anayesikiliza aelewe alibainisha kuwa mambo mengi yanahalibika kwa kuwa hofu ya Mungu imetoweka watu hawaogopi kutoa mimba kuua watoto na mambo mengi maovu. Alifafanua mambo mengi kwa kina kuhusu malezi ya Watoto, Vijana na Maisha kabla na baada ya ndoa. Mwalimu huyu amebobea sana katika mambo haya na nilitamani sana elimu watu wengi waipate ili jamii iwe na kizazi chenye mtazamo chanya wa maisha ya kila siku hasa katika kipindi hichi ambapo maadili ya kizazi chetu yameparaganyika. Ukitaka mawasiliano nae mwl huyu na kupata uhondo wa mafundisho yake > willbroad68@gmail.com Chao.




Mwl Prosper
mtaalamu wa mafundisho ya kifamilia.

Hakuna maoni: