Jumatatu, 9 Agosti 2010

TUNAJIFUNZA NINI CHAGUZI ZA NDANI YA VYAMA?

Nichue nafasi hii kuwapongeza Mh Peace Lumelezi na Mh Charles Mkama kwa kuthubutu kugombea nafasi za ubunge kwa sisi tuliokoka ni changamoto kubwa wakati Mch D Kanemba akiwapongeza katika ibada ya j2 alisema mimi nawahesabu kuwa ni washindi hamjashindwa na aliongeza kuwa watu tuliookoka ambao ni waaminifu tumejisahau sana na kusababisha nafasi nyingi za uongozi kuchukuliwa na watoto wa mama mdogo.
Kweli mimepata kitu hapa. Uchaguzi wa awali ambao umefanyika kwenye vyama ukichunguza wengi wao ni watoto wa mama mdogo hata wewe jaribu kuuliza watu ni watu wangapi waliokoka wenye kadi za vyama vya siasa do ni wachache sana kama ni hivyo ni ndoto kupata viongozi waminifu waliokoka. Je maombi ya kufunga na kuomba tu yanaweza kutupa viongozi wazuri !!! au je hivi kweli wote tuliopo makanisani tunataka kuwa wachungaji na wainjiristi? hasha nitoe changamoto kuwa tuamuke sasa tuwe na kadi za vyama siasa ili na sisi tuweze kupigia kura watu waaminifu nitoe mfano ulitokea tabora samahani kwa kutaja kanisa, Kitete ni kanisa kubwa lenye watu wengi lakini cha kushangaza watu wengi hawana kadi za vyama vya siasa hivyo hawana haki ya kuchagua mtu kwenye kura za maoni za kupata madiwani au wabunge lo inashangaza. Kwakweli sasa tunatakiwa tuamke kuhamasishane kuwa na fursa za kugombea au kuchagua. Kwa mjibu wa wagombea walioshiriki (Lumelezi na Charles) wabainisha kuwa uchaguzi ulikuwa na rusha mambo ya ushirikina na mambo mengi maovu na haitoshi tu sisi kuombea tu bali na sisi tuthubutu na tuwe na kadi za vyama.
Kweli hata mimi sina kadi ila kwa hili naenda kutata kadi na usiniulize chama gani hiyo ni siri yangu na wewe kakate ya kwako asante

Hakuna maoni: