Jumatatu, 9 Agosti 2010

Mkowa wa Tabora vamiwa na wainjilisti

Ni jambo la kufurahisha pale injili inapohubiriwa nichukuwe nafasi hii kuipongeza timu ya uinjilisti kutoka Magomeni TAG ambao kwa karibu wiki moja na nusu walikuwa wakifanya huduma katika makanisa mbalimbali katika manispaa ya Tabora kuna shuhuda nzuri za watu kufunguliwa kutoka katika vifungo vya magonjwa, na vingine mbalimbali. kikubwa cha kumshukuru Mungu ni kuwa aliweza kuonekana kwa kiwango cha juu sana na kila aliyesimama kufundisha kwa kweli Mungu alimtumia. watumishi waliosafiri kwenda Tabora ni Ev E.Kipwate kiongozi wa msafara, Ev Nelsoni Kazimoto, Mwl Ester Mbezi, Mwl Frank Mhomi Mwl W Kipwate, Mrs E kipwate na wanamaombi 2 Marther na Ayubu. kwa kweli kazi yao ni nzuri na ya kuingwa maana Yesu anatutaka tutoke tupeleke injili kwa kila kiumbe na tunapotoka ndipo tutaona uzihirisho wa nguvu za Mungu. moja ya shuhuda nilizopata ni ya mama mmoja aliyekuwa mgonjwa amelala kitandani hoi tangu Janualy 2010 na baada ya kutembelewa na timu hiyo alifunguliwa na kuwa mzima kabisa na hata kuweza kuwaandali chakula. utukufu ni Mungu wa mbinguni.
Chapisha Maoni