Kanisa la City
Worship Centre lililo chini ya Mchungaji Timothy Mwita linatazamia
kutimiza mwaka mmoja tangu kuanzishwa kwake mapema mwaka jana. Blog yetu
ilipata nafasi ya kuongea na Mchungaji huyo Kiongozi wa Kanisa hilo.
Ze Blogger: Mchungaji Kiongozi ninayo furaha kukutana na Wewe, siku ya Leo.
Pastor Mwita: Asante sana nami pia nimefurahi.
Ze Blogger: Tarehe 2 February, 2014 tunategemea nini kutoka City Worship Centre?
Pastor Mwita: Siku ya tarehe 2/2 tunategemea kuwa na Ibada maalum ya
maadhimisho (Anniversary) ya mwaka mmoja wa huduma yetu,tangu kuanza kwa
kanisa.
Ze Blogger,
hongereni sana, kumekuwa na uibukaji wa makanisa kama uyoga siku za
miaka ya karibuni na kuna madhehebu makanjanja yamekuwa yakianzishwa
kila leo, wewe Kama huduma mpya katika Jiji lenye huduma lukuki hapa
Dar-es-Salaam changamoto zipi umekutana nazo kihuduma.
Pastor Mwita: Changamoto
ya
kwanza ni utofauti wa mji na miji niliyowahi kufanya huduma kama Mwanza
na
Knjaro,mji huu watu wake wako busy sana, pia ni rahisi kuwapata
washirika wa
ktkt ya wiki mikoani sio hapa,pia watu ni watafiti sana na hii
inawafanya wachungwe na mch zaidi ya mmoja, mtu anaweza kuja kanisani
saa 3 akiwa
ameshasali makanisa hata 2 tayari,wengi hawachungwi. Pia yapo maeneo
ambayo
hayajafikiwa kabisa hapahapa mjini.,na yanahitaji huduma maalum. Eneo la
kudumu
la kuabudia ni changamoto nyingine to mention the few.
Ze Blogger: Nina amini yeye aliyekuita atakuongoza, siku ya tarehe 2 kutakuwa na nini hasa.
Pastor Mwita:Tarehe 2
kutakuwa na kipindi cha kusifu na kuabudu kwa muda wa kutosha kama desturi ya
kanisa letu,pia tutakuwa na wageni tuliowaalika toka maeneo mbalimbali ya jiji
na nje ya jiji,pamoja na waimbaji binafsi., hafla yetu itakwenda sambamba na
kuwatambua watu waliotusaidia kufikia mafanikio haya. Mwisho tutamaliza kwa
kula pamoja. Ibada zetu kwa
kawaida huanza saa 3-5, lakini kwa sababu ya umuhimu wa tukio hili tutaanza saa
2-7.
Ze Blogger: Mtu anawezaje kufika huduma hii ilipo?
Pastor Mwita: Jinsi
ya kufika kituo kikuu ni Morocco kisha unaelekea kama unakwenda Mwenge mkono wa
kulia kuna Hospitali ya AAR basi nyuma yake ndani ya Shule ya Sunrise mtaa wa
Chato- Regent Estate
Ze Blogger: asante sana pastor Mungu akubariki.
Pastor Mwita: Asante ubarikiwe na wewe
KWA HISANI YA SAMUEL SASALI
KAMA UNA MAONI YOYOTE NIANDIKIE HAPO CHINI AU TUMA UJUMBE KWENYE NO +255 715 033 671, +255 767 033 671 AU FB Martin Malecela follow me in Twetter martmalecela au tembelea page yetu na ulike martmalecela.blogspot.com
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni