Usiku wa Jumamosi ya tar. 20/04/2013 ulikuwa ni usiku wa GLORIOUS
CELEBRATION - Family Dinner. Kusudi kubwa lilikuwa ni kukutana na
waimbaji wote wa GC kwa pamoja na wazazi wao, walezi na ndugu wa karibu.
Hii pia ilijumuisha wanandoa kwa wana GC amabao wameoa au kuolewa.
Kwanza tunamshukuru Mungu kwa kibali na yote yaliyojiri. Pili
tunamshukuru mlezi na mbeba maono wa GC, wazazi na wote waliofika. Kwa
nyakati tofauti, mlezi wetu pamoja na baadhi ya wazazi walitoa mahusia
mbalimbali. Kwa hakika ulikuwa usiku wa furaha kuwaona wanaGC kuwa
pamoja na wazazi wao, ndugu jamaa na marafiki.
Ni matumaini yetu siku si nyingi tutakuwa na usiku wa wanaGC wote,
yaaani pamoja na wewe. "Tazama jinsi ilivyo vema na kupendeza ndugu
wakikaa pamoja kwa umoja ni kama mafuta mafuta mazuri yatiririkayo
kichwani mpaka kwenye ndevu za haruni" Zaburi 133:1-2.
SIFA NA UTUKUFU KWA MUNGU!
KAMA UNA MAONI YOYOTE NIANDIKIE HAPO CHINI AU TUMA UJUMBE KWENYE NO +255 715 033 671, +255 767 033 671
AU FB Martin Malecela follow me in Twetter martmalecela
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni