BAADA ya serikali kutoa Baraka zake kwa kutoa kibali kufanyika kwa Tamasha la Kimataifa la pasaka la mwaka huu lenye kauli mbiu ya ‘Amani na Upendo’ kamati ya maandalizi imeanza rasmi maandalizi yake ambapo mwaka huu linatarajiwa kuwa la tofauti kubwa. Moja ya mabadiliko hayo ni pamoja na watazamaji kupewa nafasi ya kuchagua mikoa isiyopungua mitano itakapofanyika tamasha na waimbaji watakaoimba pamoja na kuwa na waimbaji wengi wa kimataifa kutoka nje.
Alex Msama Kushoto muandaaji wa Tamasha la pasaka |
Akizungumza jijini Dar es Salaam Mkurugenzi wa Msama Promotions, Alex Msama alisema kuwa kubwa lililopo ni kuboresha Amani na upendo katika nchi yetu hivyo itakuwa kauli mbiu ya tamasha la mwaka huu kila mkoa kwa lengo la kuhimiza watanzania wote litakapofanyika kudumisha hii tuliyonayo .
Aliitaja mikoa inayopigiwa kura kuwa ni pamoja na Dar es Salaam, Mbeya, Iringa, Dodoma, Mwanza, Shinyanga , Musoma, Arusha na Kilimanjaro ambako mpenzi wa tamasha atatakiwa kupiga kura kwa kutumia simu za mikononi ataandika neno Gospo anaacha nafasi anandika mkoa anaotaka halafu anatuma kwenda namba 15522. Aidha Msama alisema kwa upande wa kuchagua waimbaji anaotaka waimbe katika tamasha anaandika neno Gospo anaacha nafasi kisha jina la mwimbaji halafu anatuma kwenda kwenye namba 15678 kila ujumbe utagharimu gharama za kawaida ya mtandao unaotumia.
“Wale wanaokuja kutazama Tamasha la Pasaka ndio watapewa kipaumbele kuchagua mikoa na waimbaji wanaotaka waimbe, hivyo tunaamini kwa kutumia utaratibu huu tutapata waimbaji wale wanaowahitaji wao kupitia utaratibu huu, na pia kutakuwa na waimbaji wakubwa wengine kutoka nje ya nchi kwa hiyo tamasha la mwaka huu litakuwa na tofauti kubwa sana na yaliyowahi kufanyika ” Asilisema Msama.
Wakati huohuo Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) limeshauri tamasha kubwa la Pasaka linalofanyika mara moja kwa mwaka, lifanyike nchi nzima badala ya mikoa michache kama ilivyo sasa.
Viongozi wa baraza hilo walisema kupunguzwa kwa mikoa inayofanyika tamasha hilo, inawafanya mashabiki wengine kunyimwa haki yao.
Wakizungumza na Dira ya Mtanzania, Mkurugenzi wa mfuko wa uwezeshaji Angelu Luhala na yule wa ukuzaji sanaa, Nsao Shalua , walisema tamasha hilo lifanyike kwa muda wa mwezi mzima katika mikoa yote kwa ajili ya kutoa burudani kwa watanzania .
“Hiki kitu ni kizuri sana tena cha kipekee sana Afrika nzima hakuna, hivyo ni vema Tamasha hili liwe la nchi nzima ili na watu wa sehemu nyingine wapate haki,” alisema Luhala.
KAMA UNA MAONI YOYOTE NIANDIKIE HAPO CHINI AU TUMA UJUMBE KWENYE NO +255 715 033 671, +255 767 033 671
AU FB Martin Malecela follow me in Twetter martmalecela
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni