Jumapili, 6 Januari 2013

UKO TAYARI KWENDA NA NABII ZA MWAKA 2013

Tunamshukuru Mungu kwa kuuanza mwaka 2013 vema kabisa. Nimejaribu kufuatilia mahubiri ya watumishi mbalimbali katika kuukaribisha mwaka wamehubiri kuwa mwaka 2013 ni mwaka wa mafanikio. Mimi nakubariana kabisa na mahubiri yao na wao kama watumishi wa Mungu kazi yao imeisha ya kusema kile ambacho Mungu amewatuma kuwaambia binadamu.

Changamoto kubwa iliyopo ni pale kuweka maneno hayo katika utendaji ili yaweze kuwa halisi wasi wasi wangu kuwa kuna uwezekano mkubwa mwaka ukaisha wengi wetu wakawa kama walivyoingia au mwaka ukawa mbaya zaidi kuliko kwaida lakini hii inatokana na ukiri wako pamoja na namna unavyoingia kwa imani katika kulifanyia kazi maneno hayo ya watumishi hao.

Nataka leo niweke angalizo ili usiwe mmoja wa watu ambao watamaliza mwaka bila kuwa na mafanikio yoyote. Ili mafanikio yaelekee kwako unatakiwa ukae vizuri na Mungu ili malaika wafanye kituo katika nyumba yako vile kuna mambo ambayo tunatakiwa kuyafahamu.

1. Kuongezeka kwako au mafanikio yako yatatokana na vile unavyotoa na si unavyopokea. Neno la Mungu linasema ni heri kutoa kuliko kupokea , hivyo tunatakiwa kutoa zaidi ili kupata zaidi. Waafrika wengi tumekuwa na mtazamo hasi katika swala la kutoa na ninakumbuka niliwahi ambiwa kuwa kama unataka kuwa tajiri unatakiwa kujibana au kubana matumizi ili uwe na akiba ya kutosha jibane katika kula , jibane kuvaa, jibane kwenye kila kitu. Kwa kipindi hicho niliamini lakini baadae nimepata mafundisho sahihi na fomula ya kimungu, na nchi nyingi zilizoendelea wana jua siri hii na ndo maana watoa san asana misaada na hawapungukiwi kamwe maana wanajua sheria ya kimungu kuongezeka kunatokana na vile unavyotoa kinachotokea sisi tunaopewa misaada kila siku tunakuwa maskini tu.

2. Unatakiwa kujua kuwa Mungu ndiye sorce ya mafanikio yetu na si vinginevyo, watu wengi wana dhali chanzo cha mafanikio yao yako katika kazi zao hivyo anawaza kuwa akiwa na kazi nzuri basi atakuwa kapata maisha , wengine wanadhani elimu kiasi kwamba wanasoma kwa bidii ili wapate mafanikio baadae, wengine wanajua kuwa chanzo mi biashara zao kubwa au miradi yao mikubwa basi ndiyo chanzo cha mafanikio yao. Wewe kama mtoto wa Mungu unatakiwa kujua mafanikio yetu chanzo chake ni Mungu mwenyewe. Wengi wana kazi nzuri na bado hawana amani, wengine wana elimu kubwa lakini bdo siyo msaada kwao wngine wana biashara na miradi mikubwa lakini wanaishi maisha ya mateso kutokana na masharti waliopewa na hao waliowasaidia kuwa na miradi hiyo.

3. Utavuna kile ulichopanda, watanzania wengi tunapenda kuwa na mafanikio makubwa lakini sisi wenyewe si wasababishaji wa hayo mafanikie wengi wetu tunataka mbambo yawe tu kama uyoga unavyoota na ugumu ndo unakuja hapo. Tunapenda kuvuna tusivyo panda sasa vile utakavyo panda ndivyo utakavyo vuna ukipanda haba utavuna haba na ukipanda mbegu nyingi utavuna mavuno mengi hivyo hivyo. Hivyo jitahidi kupanda mbegu nzuri tena kwa wingi ili uwe na mavuno mazuri

Sasa kazi kwako kuhakikisha kweli kuwa mwaka huu wa 2013 unakuwa ni wa mafanikio kutokana na vile watumishi wengi wa mungu walivyo tabiri. kama hayatatimia kosa si kwa waliotoa unabii bali ni kutokuamini hizo nabii.


KAMA UNA MAONI YOYOTE NIANDIKIE HAPO CHINI AU TUMA UJUMBE KWENYE NO +255 715 033 671, +255 767 033 671 AU FB Martin Malecela follow me in Twetter martmalecela

Hakuna maoni: