Jumatano, 26 Septemba 2012

MFAHAMU NEEMA NG'ASHA MWIMBAJI WA NYIMBO ZA INJILI

Siku za leo kuna waimbaji wa nyimbo za injili wamekuwa wengi sanaaaa na blog hii ilipata kufanya mahojiano na mwimbaji wa nyimbo za injili Neema Ng'asha Mwamba yeye anasali katika kanisa la Askofu Kameta Tabata fuata nami katika mahojiano haya ili uweze kumfahamu mwimbaji huyu.
blog hii ilifanya mahojiano nae ili kujua mambo mbalimbali yanayohusu huduma yake unangana nasi katika mahojiano hayo.

Martmalecela ; ulianza lini huduma yako
Neema Ng'asha ; nilianza kuimba mwaka 1998
Martmalecela ; kitu gani kilichokufanya kuvutiwa kufanya huduma hii
Neema Ng'asha ; sikuwa na penda kuimba hapo awali ila siku moja mungu alinigusa kwa njia ya tofauti sana nikiwa form two. sitaweza kusahau siku hiyo na tangu siku hiyo mungu aliweka huduma ya uimbaji moyoni mwangu na nikaanza kuimba kwa kweli sikushwawishiwa na mtu kuingia katika huduma hii ya uimbaji nilisikia wito kutoka kwa Mungu toka moyoni mwangu
Martmalecela ; kwa muda gani sasa umekuwa ukifanya huduma hii
Neema Ng'asha  Rasmi nilianza mwaka 2009 niliporekodi albamu yangu ya kwanza
Martmalecela ; Kuna mtu yeyote aliyekusaidia wewe kufikia hapa ulipo .
Neema Ng'asha ; Namshukuru mume wangu nissi mwamba amekuwa akinitia moyo na kunishauri katika huduma hii pia nawashuruku wazazi wangu (mr&mrs Ng'asha),Martha Ng'asha (dada)na bishop Lawrence Kameta
Martmalecela ; umeshatoa matoleo mangapi
Neema Ng'asha ; nina albamu moja tu ya audio video yake itakukamilika mwishoni mwa mwaka huu
Martmalecela ; kuna changamoto gani ambazo unakutana katika huduma yako
Neema Ng'asha ; changamoto kubwa ni wasambazaji mpaka sasa sijapata msambazaji wa kazi yangu na pia upande wa kifedha bado ni tatizo maana huduma ina hitaji pesa kwa ajili promotion na kurekodi albamu nyingine
Martmalecela ; msaada gani unaohitaji kama akitokea mtu kutaka kukusaidia nahitaji
 Neema Ng'asha ; msambazaji wa kazi yangu pia nahitaji mtu atakaye ni support kimawazo na kifedha pia
Martmalecela ; una ushauri gani kwa wanaotaka kufanya kama wewe
Neema Ng'asha ;napenda kuwashauri watu wenye huduma kama yangu wamtegemee mungu sana na waishi maisha ya utakatifu mungu atawatumia toka utukufu hadi utukufu
Martmalecela ;nyimbo zako unatunga mwenyewe au unatungiwa
Neema Ng'asha ; namshukuru mungu nyimbo zangu natunga mwenyewe mungu amekuwa mwaninifu ananipa nyimbo mpya

Mazoezi ya kupiga gitaa
Martmalecela ; kuna mwimbaji yeyete maarufu ambaye umewahi kushirikiana nae,
Neema Ng'asha ; sijahwahi kushirikiana na muimbajii yeyote maarufu

unaweza kumuarika mwimbaji huyu kufanya huduma kanisani kwako au kwenye shughuli yako unaweza kuwasiliana kwa no  0712 245986  na unaweza tembelea blog yake http://www.neemangasha.blogspot.com/

na unaweza kupata caller tune katika simu yako ya Tigo yenye nyimbo zangu andika  FP kwenda 15050 utapata wimbo "NIKURUDHISHIE NINI BWANA" na wakituma AB kwenda 15050 watapata wimbo "LORD MY GOD"
KAMA UNA MAONI YOYOTE NIANDIKIE HAPO CHINI AU TUMA UJUMBE KWENYE NO +255 715 033 671, +255 767 033 671 AU FB Martin Malecela follow me in Twetter martmalecela

Hakuna maoni: