Alhamisi, 2 Agosti 2012

MAFUNDI MITAMBO NA WAPIGA VYOMBO VYA MUZIKI MKO TAYARI???? MARK MALHERBE SOUND ENGINEER KUFUNDISHA TENA SEPT 2012

Yule Mwalimu  mbobevu wa somo la ufundi mitambo  Mr Mark Malherbe ambaye yeye ni sound engineer- prosound (pty) ltd ya South Africa kutua tena Tanzania kuwanoa mafundi mitambo wa vyombo vya muziki. amekuwa ni mbobevu katika tasnia hiyo kwa zaidi ya miaka 31 ndiye aliyefunga vyombo vya mashidano ya mpira FIFA  katika viwanja vya mpira 9 katika kombe la Dunia lililopita kule south Africa na amepewa tena kazi hiyo kwa mwaka 2014 kule Brazil. mafunzo hayo yatafanyika tena Dar es Salaam Tanzania Tar 28-29 Sept 2012
Mafunzo yaliyofanyika mwaka jana kwenye kanisa la TAG Magomeni

Waliohudhulia mafunzo ya mwaka jana watakubariana na mimi kuwa darasa hili si la kukosa maana kuna mambo mengi sana utajifunza kwa habari ya ufungaji na utumiaji wa vyombo vya muziki. yeye alifunga vyombo katika viwanja vya mpira kule South waliweza kufunga reki 156 ambazo zina Power Amplifier 3000 hivi, mafundisho yake yaliwavutia watu sana na kusababisha watu kuona muda wa mafunzo ni mdogo hata likazaliwa wazo la kufungua chuo cha ma sound engineer hapa Tanzania ambacho kitasimamiwa na yeye kwa kushirikiana na VHM.
Umati wa watu waliohudhulia mafunzo mwaka jana mwaka huu nadhani ukichelewa unaweza kosa nafasi wahi sasa mapema
Tarifa nilizozipata kutoka VHM kuwa mwalimu huyo atakuwa hapa nchini katika tar zilizotajwa hapo juu kwa mafunzo ya siku 2 tu. katika siku hizo 2 kila mtu anayetaka kuhudhulia mafunzo hayo anatakiwa kulipia sh 30,000. tu na baada ya mafunzo utapata cheti. mafunzo hayo yatafanyikia katika kanisa la TAG mwenge. pamoja na mwalimu huyo pia atafuatana na mwalimu mwenzake ambaye yeye ni mtaalamu wa Praise and worship Rev Gary Rivas (senior pastor Gracepoint church south Africa ambaye yeye ana kanisa la washirika 3000 ndani ya miaka 7.

nakumbuka mwaka jana kuna watu walitoka mikoani na nchi za jirani kama Kenya kuja kupata mafunzo hayo itakuwa kosa sana kwa wewe mtu wa Dar kukosa.

habari ya mwaka jana hii hapa http://martmalecela.blogspot.com/2011/10/vhm-yawaondoa-mafundi-vishoka-na.html?spref=fb

anayetaka kuhudhulia aanze kufanya maandalizi mapema kabla nafasi hazijaisha unaweza wasiliana na waandaaji ambao ni VHM 0715 237 789

 KAMA UNA MAONI YOYOTE NIANDIKIE HAPO CHINI AU TUMA UJUMBE KWENYE NO +255 715 033 671, +255 767 033 671 AU FB Martin Malecela follow me in Twetter martmalecela

Hakuna maoni: