Jumapili, 16 Oktoba 2011

VHM YAWAONDOA MAFUNDI VISHOKA NA MAKANJANJA KWA KUTOA ELIMU

Kongamano la mafundi mitambo wa vyombo vya music na viongozi wa kwaya na praise team limemalizika leo kwa mafanikio makubwa, zaidi ya washiriki wapatao 400 wametunukiwa vyeti katika mafunzo hayo. Kongamano hilo lililoandaliwa na VHM na The global leadership summit likuwa ni kongamano la aina yake kufanyika hapa Tanzania akiongea mbele za mgeni rasmi aliyemuwakilisha waziri wa utamaduni na michezo pastor Peter mitimingi kumekuwa na upungufu mkubwa wa mafundi mitambo wenye elimu katika taasisi mbalimbali ikiwemo makanisa, mikutano, kumbi mbalimbali nk hivyo kusababisha kupata hasara ya mamilioni ya pesa kwa vyombo vinavyoungua au kuharibika baada ya kukosewa kuunganiswa. Kwa kutambua hilo VHM ikishirikiana na marafiki zao wakaona walete wataalamu waliobobea katika fani hizo ili watoe elimu.


Nikiwa mmoja wa watu niliohudhulia mafunzo hayo nilivutiwa na walimu waliofundisha ambao ni wabobevu somo la ufundi mitambo lilifundishwa na Mr Mark Malherbe ambaye yeye ni sound engineer- prosound (pty) ltd South Africa ambaye yeye amekuwa ni mbobevu katika tasnia hiyo kwa zaidi ya miaka 30 akielezea wasifu wake alisema yeye ndiye aliyefunga vyombo vya souti katika viwanja vya mpira 9 katika kombe la Dunia lililopita kule south Africa na amepewa tena kazi hiyo kwa mwaka 2014 kule Brazil alizidi kusema katika uwanja mmoja tu waliweza kufunga reki 156 ambazo zina Power Amplifier 3000 hivi, mafundisho yake yaliwavutia watu sana na kusababisha watu kuona muda wa mafunzo ni mdogo hata likazaliwa wazo la kufungua chuo cha ma sound engineer hapa Tanzania ambacho kitasimamiwa nay eye kwa kushirikiana na VHM.

Vilevile kulikuwa na mwalimu aliyefundisha somo la praise and worship Rev Gary Rivas (senior pastor Gracepoint church south Africa ambaye yeye ana kanisa la washirika 3000 ndani ya miaka 7 tu naye somo lake lilikuwa zuri sana. Mafunzo hayo yalihudhuliwa na wanafunzi kutoka sehemu mbali mbali za Tanzania na nchi jirani ya Kenya na kongamano hilo lilipambwa na bendi ya messengers na kuhudhuliwa na waimbaji wengi wa nyimbo za injili na wadau wa vyombo vya mziki wa kanisani na duniani.

Mafunzo hayo yaliyofanyika katika kanisa la TAG Magomeni kwa kweli lilifana na kumalizika kwa wahitimu wote kupewa vyeti na kuuziwa DVD zenye mafunzo hayo ili wanafunzi wakajifunze wenyewe, akuwa yakifanyika kila mwaka ili kuondoa mafundi vishoka na makanjanja. Wanafunzi wote walikabidhiwa vyeti na katibu wa wizara ya michezo na utamaduni kwa niaba ya waziri.

Waimbaji wa Mesenger's Band wakiimba katika kongamano

 
Walimu wa mafunzo wakifuatilia jambo kushoto ni Rev Gary Rivas na Mar
k
Mapacha wawili wakifanya huduma Pastor Mitimingi na Pastor Abel
Amoni Akikumbuza enzi za amana kwa kupiga wimbo wa cha kutumaini.


wakongwe wakiimba wimbo wa cha kutumaini

Pastor Abeli akiiongoza wimbo wa chakutumaini.

Hakuna maoni: