waumini wa kanisa AG Iran wakiwa kanisani kabla ya ibada zao kuzuiwa |
vikosi vya askari wa Revolutionary Guard's Intelligence, vilivamia kanisa hilo na kutoa amri ya kufungwa kwa kanisa hilo, na kufanya nchi hiyo kubaki na makanisa matatu tu ambayo yana tumia Lugha ya farsi yaliyopo katika mji wa Tehran. makanisa yaliyobaki ni Assemblies of God Central church of Tehran, ambalo pia limekuwa likikubwa na misukosuko mara kwa mara na Presbyterian na lile la kiinjilisti. aidha kabla ya amri hivyo makanisa yaliamuriwa kubadilisha ratiba za kusali kutoka Ijumaa (ambayo ni siku ya mapumziko kwa nchi ya Iran) hadi Jumapili(ambayo ni siku ya kazi) kwa lengo kuwa watu wengi hawataenda kanisani maana watakuwa kazini.
waumini katika nchi ya Iran na nchi nyingine za kiislamu maisha yao na familia zao yanakuwa katika wakati mgumu, tunatakiwa kuingilia kati hali hii kwa maombi, alisema Bw Greg Mundis, ambaye ni Mkurugenzi wa idara ya umisheni katika kanisa la AG makao makuu, na kuongeza, yatupasa kuingilia kati kwa imani ili kuwaokoa kaka zetu na dada zetu ambao wanateseka kwaajili ya jina la Yesu Kristo. amri ya kufunga kanisa inakuja baada ya ile ya kufunga kanisa lingine lililokuwa katika mji wa Ahvaz iran ambalo liliambatana na kukamatwa kwa waumini wote na kuhojiwa. japo yapo makanisa ya nyumba kwa nyumba ambapo waumini hukutanika kwa siri kubwa.
miezi michache iliyopita kiongozi mkuu wa shirika la AG duniani Askofu DK George Wood alikutana na Rais Barrack Obama wa Marekani kumuomba aingilie kati kuiasa serikali ya kiislamu ya Irani kumwachia Huru watu zaidi ya 20 ambao wako kizuizini kwa kosa la kuacha uislam na kujiunga na ukristo na kuwashawishi na watu wengine kuwa wakristo. katika taarifa yake bw Wood aliongeza inatupasa kuendelea kuwafahamisha viongozi wetu wa kisiasa juu ya mateso ambayo ndugu zetu wanakabiliana nayo katika sehemu mbalimbali za Dunia hii, na tuviombe vyombo vya habari vya wenyeji kuwa makini ili kuripoti matukio yote ya ukandamizwaji wa haki za binadamu na uhuru wa kuabudu kila kona hapa Duniani.
KAMA UNA MAONI YOYOTE NIANDIKIE HAPO CHINI AU TUMA UJUMBE KWENYE NO +255 715 033 671, +255 767 033 671 AU FB Martin Malecela follow me in Twetter martmalecela
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni