Benny Hinn |
Benny na Suzan |
Wakati akiwa
Marekani kwenye mkutano wa
miujiza uliofanyika alhamisi usiku tar 31 May,
Benny Hinn alitangaza kuwa amefanya mapatano ya kurudiana na mke wake, Suzanne.
“Mchungaji Benny aliwaambia usiku ule” Maurice
Sklar muanzilishi wa huduma ya Maurice Sklar, aliiweka habari hii kwenye
ukurasa wa facebook. “kuwa Benny na Suzanne wamepatana! Benny alisema kuwa
watafunga pingu za maisha kwa mara nyingine mwezi wa kumi na mbili! Maurice anasema alivyosikia habari hiyo nusura
aanguke kutoka kwenye kiti alichokuwa amekalia. Hakika huyu ni Mungu wa maajabu,
alisema HUU NI MUUJIZA! Bwana Yesu asifiwe, nina furaha kubwa sana kusikia
habari hizi!”
Baada ya miaka zaidi ya 30 ya ndoa, Suzanne aliomba
apewe hati ya kuachwa ( taraka) mwezi wa Februari 2010 akikataa kuendeleza
mahusiano yao kutokana na kutofautiana. Kwa wakati huo Benny Hinn alitoa taraka
akisema “Nimeshitushwa na kufadhahishwa na habari hii sikuwa na taarifa yeyote
ya awali”
Pamoja na kurejesha mahusiano yao, Suzanne
alishangazwa kusikia habari ya tarehe yao ya kufunga ndoa kwa mara nyingine.
Haya yalisemwa na ndugu wa karibu na familia hiyo katika kituo cha habari cha
Charisma, “Tangazo hili lilikuwa ni la awali, lakini endelea kuliombea jambo
hili,”
Baada ya Suzanne kujaza hati ya kuachwa, Benny Hinn
alikiri kuwa amechangia kwa kufa kwa ndoa hiyo kwa kuwa karibu sana na huduma
yake kuliko familia. Alisema kuwa mara nyingi nilikuwa nafanya huduma ya
kuhubiri kwanza, nikitambua fika mafundisho niliyokuwa nafundisha yalikuwa
yakiwaumiza watoto wake.
Hii ni habari njema nikijua kuwa itakuongezea
Baraka na kukutia moyo katika familia yako. Mungu wetu ni Mungu uhuisho na
matengenezo. Msalaba ni alama kubwa ya kuonyesha na kudhihirisha kuwa yeye ni
Mungu anaye wapatanisha watu, na ndilo tumaini pekee la uponyanyi wetu.
Nafahamu, kwakuwa ninauzoefu na uponyaji tangu nilipo yakabidhi maisha yangu
kwa Yesu kwa miaka mingi iliyopita; lakini nimekuwa nikiufahamu mguso wa
uponyaji wake kwa kipindi cha sasa alipoanza kuuonyesha utukufu wa uponyaji
wake katika familia yangu, katika hatua za kuiuhisha ndoa yangu. Na uponyaji
huu ulianza tangu sikukuu ya Krisimasi.....haikuwa krisimasi ya kuwa mpweke,
maisha yangu yalibadilika kitofauti kuliko ilivyokuwa awali. Watoto wangu,
wajukuu, na Suzanne kwa pamoja tulikutana siku ya krisimasi. Nilianza kuhisi
kuwa Mungu ameanza kutembea katikati ya familia yangu nakuleta uponyaji wa
uhuisho kwa maombi niliyo omba kwa muda mrefu. Tulicheka pamoja, kubadilishana
zawadi, na kukumbushana maajabu mengi yakifamilia kwa miaka iliyopita, na
niliomba maombi mepesi, “Bwana Yesu ilinde familia yangu kwa utukufu wa jina
lako.” Kama wengiwenu mnavyofahamu, mke wangu, Suzanne tumekuwa na kipindi
kigumu sana katika maisha yetu ya ndoa. Siku jiandaa kutangaza kwa kile
kinachotaka kutokea, lakini na waombeni endeleeni kuiombea familia yangu, na
pia endeleeni kuangalia kipindi cha televisheni cha Hii ni siku yako kwa habari
ambazo Mungu atafanya.
Lakini
nitaeendelea kusema, ninacho hitaji zaidi kuliko chochote ni mapenzi ya Mungu
yafanyike katika maisha yangu, maisha ya Suzanne, kwa watoto wangu, na kwa
wajukuu wangu. Kama familia tumekuwa mbalimbali
sana, lakini tumemuona Mungu akiwaita binti zangu kumtumikia, kumuokoa
kijana wangu, na sasa yuko kwenye hatua ya kuhuisha ndoa yangu.
Wapendwa
wangu naomba niwaambie kwamba kuhubiri injili ya Yesu ni moyo wangu, na ndo
maisha yangu, na ninataka niendelee kuhubiri mpaka pale mapigo ya moyo wangu
yatakapo koma. Nataka niliseme neno, “Yesu anaokoa, Yesu anaokoa, Yesu anaokoa”
mpaka moyo wangu utakapo koma, kwa utukufu wa jina lake. Mmekuwa marafiki na
ndugu zangu kwa kipindi chote, kwa yote yaliyotokea, kwa moyo wangu wote nasema
asante, asante, asante. Pia namshukuru Mungu wangu kwa kuwaleta wote katika
maisha yangu, nianomba awabariki zaidi
na zaidi, awape yote mnayo hotaji katika maisha yenu. Nina wombeeni kila siku,
Mungu aponye maisha yenu, vyanzo vya fedha.
Endelea
kuomba pamoja name kwamba kazi ya uponyaji wa familia yangu ukamilike, na
haraka sana tutafurahi pamoja kwa lile atakalo lifanya Mungu. Nawapenda sana sana, ninyi ni watu wapekee kwangu naweza sema.
KAMA UNA MAONI YOYOTE NIANDIKIE HAPO CHINI AU TUMA UJUMBE KWENYE NO +255 715 033 671, +255 767 033 671 AU FACEBOOK Martin Malecela follow me in Twetter martmalecela
Maoni 2 :
Hakika hii ni habari njema sana. Tena ni injili tosha. Mungu azidi kuwasaidia ili hila za mwovu shetani zibomoke vipandevipande na kutoweka kabisa kwa jina la Yesu!
Habari njema sana, Mungu azidi kuonekana katika yote wanayotarajia
Chapisha Maoni