“BWANA akamwambia Musa, Tazama, mimi naja kwako katika wingu zito ili
watu hawa wasikie nitakaposema nawe, nao wapate
kukuamini wewe nawe hata milele. Musa akamwambia BWANA hayo maneno ya
watu” (Kutoka 19:9).
Kama kuna jambo linaweza
kukuumiza maishani ni kupoteza KUAMINIWA, hasa kuaminiwa na watu wa KARIBU.
Kumwamini mtu sio kitu rahisi, ila ni rahisi kupoteza imani kwa watu kwa jambo
moja tu, tena la kijinga kabisa na lisilo na tija yoyote ya maana!
Fiki unafanya jambo kwa
kumaanisha kabisa, kwa roho safi, lakini watu hawakuamini! Unasema KWELI
kabisa, lakini watu wanaona UNAWADANGANYA tu! Tena wanakukebehi; Kumbe! Ni kwa
sababu ulipoteza uaminifu wako kwao! Hiyo inauma sana. Hapo ndipo
utaelewa umuhimu wa KUAMINIWA na watu.
Sio kila mara utaaminiwa
kwa maneno au matendo yako peke yake, Kuna wakati unahitaji msaada wa “mwingine” ili uaminiwe. Mungu akaona
afanya jambo maalumu ili Musa aaminiwe na watu milele!
Halikadhalika, hata sisi
tunahitaji Mungu au watu wengine watusaidie kuaminiwa kwetu.
Kwa mfano, usipuuze mtu anayeweza kusema habari zako nzuri mbele ya
watu wengine, hasa kama ukiwa haupo, huyu anaongeza imani ya hao watu kukuamini
wewe. Kwa upande mwingine, mtu akisema habari zako mbaya kwa watu
wengine, huyo amekufanyia uharibifu mkubwa; hasa akiwa ni mtu wako wa karibu.
Imani yao kukumini wewe inaathirika; hata kama una majina yako matukufu,
hutaaminiwa tena.
Mara nyingi sana
watumishi wa Mungu wanadhani kigezo cha kumtumikia Mungu pekeyake kitawapa
KUAMINIWA au KUHESHIMIWA na watu! Ndio maana unaweza kukuta mtu akijitetea, “mimi ni mchungaji”, “mimi ni mtumishi wa Mungu”, nk., lakini
watu hawawaamini hata kwa maneno yao mazuri!
Mungu alijua watu
wanamwamini Yeye kama Mungu, lakini aliona UMUHIMU wa Musa mtumishi wake “naye”
kuaminiwa na watu! Safari hii, Mungu alishuka katika wingu ili watu wamwamini
Musa, sio watu wamwamini Mungu.
Sasa angalia jambo hili,
Musa hakuomba neno hili; Mungu ndiye aliona afanye hivyo kwa MASLAHI ya Mungu
sio kwa maslahi ya Musa, japo anayeaminiwa hapo ni Musa!
#Frank_P_Seth
KAMA UNA MAONI YOYOTE NIANDIKIE HAPO CHINI AU TUMA UJUMBE KWENYE NO 0784 477775 au Whatup 0784 477775 AU FB Martin Malecela follow me in Twetter martmalecela au tembelea page yetu na ulike martmalecela.blogspot.com
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni
Mawazo yako ni muhimu sana tafadhali tumia lugha nzuri na tutairusha na wengine waisome.