“Waheshimu baba yako na mama yako; kama BWANA, Mungu wako,
alivyokuamuru, siku zako zipate
kuzidi, nawe upate kufanikiwa
katika nchi upewayo na BWANA, Mungu wako” (Kumbukumbu la Torati 5:16). Siku
zako kuongezwa na kufanikiwa katika mambo yako, kwa ujumla tunaweza kuita hiyo
ni baraka.
Kuwaheshimu wazazi (baba na mama
yako) ni AMRI.
Maana halisi ya AMRI ni AGIZO
ambalo likikiukwa kuna ADHABU. Ukisikia amri maana yake huna UCHAGUZI wa
kufanya KINYUME na AMRI hiyo.
Katika KUWAHESHIMU baba na mama,
kuna mtihani mkubwa kwa maana HESHIMA haipimwi na ATOAYE ila APOKEAYE. Hata
ujitahidi vipi, kama “roho” ya apokeaye hiyo heshima HAIKURIDHIKA na kiwango
cha heshima hiyo, bado haihesabiki kwakwe kama heshima hata kama umejitahida
sana.
Nimekutana na watu wakidai
wanawaheshimu wenzao ilihali wenzao wanalalamika hawaheshimiwi! Katika
kutafakari sana maana halisi ya heshima, na sababu za kujua kama mtu
amekuheshimu au la, nikakutana na mistati hii:
“1 Ikawa Isaka alipokuwa mzee, na macho yake yamepofuka asione, akamwita
Esau, mwanawe mkubwa, akamwambia, Mwanangu. Naye akamwitikia, Mimi hapa.
2Akasema, Tazama, sasa mimi nimekuwa mzee, wala sijui siku ya kufa kwangu.
3Basi, nakuomba, chukua mata yako, podo lako na upinde wako, ukaende nyikani
uniwindie mawindo; 4ukanifanyie chakula kitamu namna ile niipendayo, ukaniletee, ili nile; na roho yangu ikubariki, kabla
sijafa” (Mwanzo 27:1-4).
Isaka anasema, “ukanifanyie chakula kitamu namna ile niipendayo,
ukaniletee, ili nile; na roho yangu ikubariki, kabla sijafa”, maana yake ni
kwamba, kuna NAMNA ambayo (ile) MTU akifanya jambo, ROHO ya yule aliyefanyiwa
inatoa baraka! Baraka hazitoki mdomoni; japo zinapita mdomoni.
Sasa angalia, imekupasa kujua
namna “ILE” ya kuwafanyia wazazi wako mambo fulani ili “roho zao zikubariki”.
Mtihani huu ni wa kila mtu pekeyake kabisa. Kila mzazi anahitaji vitu fulani
kwa NAMNA ya tofauti na mzazi mwingine. Ili upate hizi baraka za wazazi wako,
imekupasa KUFANYA sawasawa na WAPENDAVYO.
Kazi ya hizi baraka za wazai ni
mbili: KUZIDISHIA umri wako na KUFANIKISHA mambo yako (kukustawisha).
Kumbuka jambo hili, wazazi wako
wapo kwa kitambo tu, hunao siku zote. Kama wapo, usiwe mvivu, maana ipo siku
utatamani kuwafanyia kitu na kumbe! Hawapo.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni
Mawazo yako ni muhimu sana tafadhali tumia lugha nzuri na tutairusha na wengine waisome.